Zuchu Atoa Ushauri kwa Wasanii Chipukizi Wanaotaka Kujikuza Kimuziki

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka WCB Zuchu amejitokeza na kuwapa wasanii chipukizii ushauri utakaowasaidia kujenga taaluma yao ya muziki. Zuchu akizungumza wakati wa mahojiano na mwanahabari kutoka Kenya Mzazi Willy M Tuva pia alisimulia safari yake ya muziki toka akiwa mchanga.

Soma Pia: Zuchu Afichua Siri Inayoleta Mafanikio Makubwa Kwa Wasanii wa WCB

Zuchu akiwa msanii ambaye alipitia changamoto chungu nzima akianza safari yake ya muziki na hata kwa wakati mmoja kukaribia kukataa tamaaa, alikuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza na wasanii wachanga ambao labda hawana matumaini kuwa watapata mafanikio kimuziki.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anavuma na ngoma yake ya ‘Nyumba Ndogo’ aliwashauri wasanii kutumia kile kidogo walicho nacho kusudi kujijenga kiusanii. Aliongeza kuwa ni vyema msanii kufanya kile ambacho kipo ndani ya uwezo wake na si kujihukumu kwa makubwa ambayo hayawezi.

Alisisitiza kuwa msanii anayejiaminia kamwe asiwahi kata tamaa kwani mafanikio yatakuja tu ingawa itabidi wakue wenye subira. Zuchu alisema kuwa kila msanii anafaa kuwa na subira kwani Mungu ndiye mwenye mipango ya wakati wa mafanikio.

Soma Pia: Zuchu Asimulia Alivyokaribia Kuacha Muziki Akiwa WCB

"Mimi niwaambie tu, Mwenyezi Mungu ana muda. Na Mungu ana muda sahihi kwa ajili yako wala usikate tamaa. Anza na uliko na uwezo kwa maana hujui nani anakuangalia. kama ni cover fanya cover kama unaeza ku record, record kwenye studio yoyote mbayo unaweza," Zuchu alisema.

Zuchu pia alisumulia jinsi alikuwa katika lebo ya WCB kwa muda wa miaka minne kabla ya kupata fursa ya kuchipuka.

Leave your comment