Zuchu Asimulia Alivyokaribia Kuacha Muziki Akiwa WCB

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Zuchu bila shaka ameingia katika rekodi ya wasanii waliopata mafanikio makubwa sana ndani ya muda mfupi katika tasnia ya burudani ya Tanzania. Akiwa na miaka ishirini na saba tu, Zuchu tayari ashakuwa msanii mwenye ushawishi mkubwa sana ndani na nje ya Tanzania.

Ila kabla ya mafanikio yake, Zuchu alipitia changamoto chungu mzima katika safari ya muziki alipokuwa msanii chipukizi. Wasichokifahamu wengi ni kuwa Zuchu alikuwepo katika lebo ya WCB kwa takriban miaka minne kabla ya kupata umaarufu na kuchipuka.

Soma Pia: Zuchu Afichua Siri Inayoleta Mafanikio Makubwa Kwa Wasanii wa WCB

Katiki muda huo wa miaka minne, Zuchu alikuwa akijitahidi vilivyo ili ajijenge kimuziki. Ila juhudi zake hazikuwa zenye matunda. Akizungumza katika mahojiano na mwanahabari wa Kenya Mzazi Willy M Tuva, Zuchu alisimulia jinsi alikaribia kukata tamaa na kuacha muziki.

Kulingana na Zuchu, kulikuwa na kipindi ambacho alihisi kuwa nyota yake haikuwa kwenye muziki. Hata kwa wakati mmoja akamwomba mamake Khadija Kopa ambaye pia ni mwanamuziki, amrudishe shuleni badala ya kuzidi kupambana na muziki.

Soma Pia: Ben Pol Asimulia Masaibu Aliyopitia Kwenye Tamasha lake la Kwanza Kabisa

Kuna wakati Zuchu alifika mwisho na kukata tamaa katika muziki. Ila kabla ya kuipa muziki kisogo, alisema wacha atie sauti yake kwenye wimbo moja ya mwisho na aende zake. Wimbo huo ilikua ‘Nadekezwa’ ambayo ilikuwa ishaimbwa na Mbosso.

Usimamizi wa WCB ulipendezwa na kazi hiyo na kisha Diamond Platnumz kibinafsi akamuarifu Zuchu kuwa muda wake wa kuwa staa ulikuwa umewadia.

"Nilikuwa nimekata tamaa kabisa. Nalia, namuambia mama nirudi shule, niache tu muziki. Lakini kakangu nisikudanganye, kikubwa mimi nilikuwa natia imani. Mwenyezi Mungu anasema Imani ndogo hata kama punje ya mbegu gani sijui wanaitaje, inatosha kukusukuma," Zuchu alieleza.

Leave your comment