Ben Pol Asimulia Masaibu Aliyopitia Kwenye Tamasha lake la Kwanza Kabisa

[Picha: Ben Pol Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii hupitia changamoto mingi sana katika safari zao za muziki kabla ya mafanikio na hatimaye kujijengea jina. Ni kupitia changamoto hizo ambazo wasanii wanapata mafunzo yatakayo wajenga kisanaa.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Benpol Aachia EP Mpya ‘B’

Msanii tajika Ben Pol kutoka Tanzania katika mahojiano ya hivi karibuni alisimulia tukio ambalo alipitia akiwa msanii chipukizi. Ben Pol alisimulia jinsi alivyopanda jukwaani kuwatumbuiza mashabiki kwa mara yake ya kwanza. Kulingana na Ben Pol, hakuwa amejifunza mengi kuhusu sanaa ya kuwatumbuiza mashabiki akiwa jukwaani.

Akizungumza katika mahojiano na Wasafi FM, Ben Pol alikiri kuwa kwa wakati huo yeye alidhani msanii ni kuimba tu, ila hakujua mengi katika dunia ya utumbuizaji.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Bob Junior Aachia ‘Itetemeshe’ Akimshirikisha Lava Lava [Video]

"Ilikuwa show yangu ya kwanza, wakati mimi naanza kuimba nilikuwa sijawaza kuhusu performance. Mimi nilikuwa najua kwamba niimbe nisikike baas, lakini sikuwa najuwa kuwa dunia ya show ni dunia tofauti," Ben Pol alieleza.

Ben Pol alikiri kuwa tamasha yake ya kwanza ilikuwa ya kuwachosha mashabiki sana. Msaani huyo alisema kuwa tamasha haikuwa ya kufurahisha licha ya kuwa wakati huo alikuwa amefanikiwa kupata ngoma iliyokuwa inavuma sana.

Ben Pol hivi maajuzi aliachia EP yake ambayo kufikia sasa imepokelewa vyema. Ben Pol akama msanii alipata mafanikia makubwa na umaarufu kupitia ngoma yake ya Moyo Mashine na nyinge nyingi.

Leave your comment