Nyimbo Mpya: Benpol Aachia EP Mpya ‘B’

[Picha: Ben Pol Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Baada ya kuchukua likizo kwa muda kidogo, hatimaye mwanamuziki Benpol kutokea nchini Tanzania amerudi kwa kishindo akiwa na EP yake mpya inayoitwa ‘B’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Damian Soul Aachia EP Mpya ‘Mapopo

EP ya ‘B’ imesheheni nyimbo nne ambazo ni ‘Kisebusebu’ aliyomshirikisha Billnas, ‘For You’, ‘Unaita’ pamoja na ‘Warira’ wimbo ambao aliuachia rasmi siku kadhaa kabla ili kusindikiza EP yake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Video ya ‘Jealous’ Akimshirikisha Mayorkun

Kimashairi, ‘B’ ni EP iliyobeba maudhui ya kimapenzi kwani nyimbo zilizomo za kwenye EP hii zinaongelea masuala kama kuachana kwa wapenzi, kukosa msimamo kwenye mahusiano, uraibu na masuala mengine mengi yanayorandana na hayo.

Katika wimbo wa kwanza kwenye EP ‘Kisebusebu’, Benpol anamzungumzia mpenzi wake ambaye hana msimamo linapokuja suala la mahusiano. Kwenye moja ya mstari Benpol anaimba "Mara nataka nawe, mara sitaki nimeghairi, mara nataka tuoane mara ngoja kwanza subiri."

https://www.youtube.com/watch?v=sTKeFi-KRF4&pp=sAQA

Ndani ya wimbo wa ‘For You’, Benpol kwa sauti ya dhati kabisa anamshukuru mpenzi wake wa zamani kwa nyakati walizopitia pamoja japo hawataweza kurudiana tena. "Ukipata muda tuongee nikusalimu si kwa ubaya natamani nikwambie nikushukuru japo kwa haya," anaimba Benpol.

https://www.youtube.com/watch?v=_B-kPIovIMI&pp=sAQA

Kwenye ‘Unaita’, Benpol anabadilika kidogo kwa kuweka vionjo vya rhumba na muziki wa zilipendwa huku kimashairi wimbo mzima Ben anatumia ustadi mkubwa kuonesha jinsi anavyofurahia mahusiano yake ya sasa. Aidha, anamsifia mpenzi wake kwa urembo alionao. Ben anaimba "I say baby Unaita, kwa tabasamu lako unaita hata ukinuna unaita."

https://www.youtube.com/watch?v=1_NV1PP0-2c&pp=sAQA

Benpol anafunga pazia la EP na ‘Warira’ amabao ni  wimbo wa simanzi. Ukisikiliza kwa umakini hata sauti ya Benpol inaishiwa nuru kwenye wimbo huu ambao Benpol analalamika kuwa hawezi kumsahau mpenzi wake wa zamani na yuko tayari hata kuacha pombe na sigara ili arudiane nae. "Kama shida pombe niko tayari kuacha aje tuyamalize si sawa mi kuniacha."

https://www.youtube.com/watch?v=VvDjAAkKd3o

Leave your comment