Nyimbo Mpya: Damian Soul Aachia EP Mpya ‘Mapopo’

[Picha: Flickr]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Damian Soul mwanamuziki anayefanya vizuri sana nchini Tanzania hatimaye ameachia EP yake iliyosubiriwa kwa hamu sana inayokwenda kwa jina la ‘Mapopo’.

Kitu cha tofauti kuhusu EP ya ‘Mapopo’ ni kuwa imesheheni nyimbo nne na nyimbo zote ni za Amapiano.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Video ya ‘Jealous’ Akimshirikisha Mayorkun

Nyimbo zilizopo kwenye EP hii ni ‘Siri’ aliyomshirikisha Nhlonipho na Leon Lee, ‘Kaserereka’, ‘Mapopo’ aliyomshirikisha Nlonipho pamoja na ‘Inanuka’.

Kwenye EP hii, Damian Soul ameonesha ufundi wake wa kuimba lugha tofauti tofauti kwani ametumia Kiswahili, Kiingereza na baadhi ya lugha kutokea Afrika Kusini.

Hii inamfanya Damian Soul kuwa msanii wa kwanza kutokea nchini Tanzania kutoa EP iliyosheheni nyimbo za Amapiano tupu bila kuhusisha aina nyingine ya muziki.

Soma Pia: Rayvanny Vs Mbosso:Nani Mkali Zaidi?

EP ya Mapopo inazidi kutoa ishara kwamba kwa sasa muziki wa Amapiano umekuwa ni muziki pendwa sana Tanzania kwani wasanii kama Diamond Platnumz, Harmonize, Ommy Dimpoz, Ney wa Mitego, Marioo na Baba Levo wameshafanya aina hii ya muziki.

Jarida maarufu la muziki duniani Billboard limeeleza kuwa muziki wa Amapiano unatoa asili yake kwenye muziki wa ‘Kwaito’ uliotamba sana kwenye miaka ya 90 huko nchini Afrika kusini lakini muziki huu uliibuka na kuanza kutambulika rasmi mwaka 2012 huko Pretoria na kufikia mwaka 2020 umetamba kwenye sehemu tofauti tofauti barani Afrika.

https://www.youtube.com/watch?v=0kzQRY1H-kY

Leave your comment