Rayvanny Vs Mbosso:Nani Mkali Zaidi?

[Picha: Biggest Kaka]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kwa sasa wakitajwa wasanii wanaofanya vizuri zaidi kwenye Bongo Fleva haitakuwa haki ukiwaacha Rayvanny na Mbosso ambao wote wapo kwenye lebo moja ya WCB. Mara kadhaa Rayvanny amekuwa akisifiwa na mashabiki kwa kipawa chake cha kufanya vitu vingi kwenye muziki kama kurap,uandishi mzuri wa nyimbo na sauti iliyotukuka huku Mbosso amekuwa ni kama nyota ya jaha kutokana na uwezo wake wa kuimba nyimbo za mapenzi zinazokosha hasa jinsia ya kike.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Sweet’ Akimshirikisha Guchi

Rayvanny na Mbosso wapo chini ya usimamizi wa Diamond Platnumz na makala hii inaangazia sehemu mbali mbali ya muziki wao:

Tuzo

2016 Rayvanny aliitwa kushiriki kwenye tuzo za MTV Africa kama msanii chipukizi, lakini alikosa tuzo hiyo. 2017 alitajwa kwenye tuzo kama AEUSA, Afrimma na kubwa kabisa ni pale aliposhinda tuzo ya BET mwaka huo huo. Mbosso kwa upande wake mwaka 2020 alishinda tuzo kama msanii bora chipukizi Afrika kwenye tuzo za Hipipo zilizofanyika nchini Uganda.

Uzoefu

Mbosso alianza kuwa maarufu kupitia Kundi la ‘Yamoto Band’ lilioanzishwa mwaka 2013. Kwenye kundi hiyo, alitumia jina la Maromboso na alipata umaarufu mkubwa baada ya kundi hilo kuachia nyimbo kama ‘Nitakuwelepweta, ‘Cheza kwa Madoido’, ‘Nisambazie Raha’, ‘Niseme’ na nyinginezo nyingi ambazo zilifanya vizuri kabla ya kundi hilo kuvunjika 2017. Kwa upande wake, Rayvanny alipata umaarufu baada ya kujiunga Wasafi 2016 na kutoa kibao chake cha ‘Kwetu’ kilichofanya Tanzania itambue umaridadi wake.

Soma Pia: Diamond Platnumz na Rayvanny Wadokeza Ujio wa Wimbo Wao Mpya

Mitandaoni

Kwenye Instagram, Rayvanny ana wafuasi milioni sita nukta tisa huku Mbosso ana wafuasi milioni nne nukta tano. Upande wa mtandao wa Twitter, Rayvanny ana wafuasi laki moja na elfu kumi na moja huku Mbosso ana wafuasi elfu ishirini na sita.

Ubalozi wa Makampuni

Septemba mwaka 2020, Mbosso alitawazwa kuwa balozi wa kampuni ya Tanga Freshi inayohusika na kusambaza na kuuza maziwa nchini Tanzania. Kwa upande wa Rayvanny pamoja na ushawishi mkubwa aliokuwa nao, mpaka sasa hajatia wino kuwa balozi wa kampuni yoyote.

Albamu

Tukiangazia wasanii hao wawili tangu wajiunge wa WCB, Rayvanny ameachia albamu moja yenye jina ‘Sound From Africa’. Mbosso pia ana albamu moja yeye jina ‘Definition of Love’.  Sambamba na hilo ni kuwa Mbosso hajawahi kutoa EP, lakini Rayvanny Januari ya mwaka 2020 alitoa EP yake inayokwenda kwa jina la ‘Flowers’.

Usimamizi

Rayvanny tayari ameshaanzisha kampuni yake ya kusimamia wasanii iitwayo Next Level Music. Mpaka sasa hajatambulisha msanii yeyote lakini bila shaka watu wanasubiri kwa hamu sana. Kwa upande wake, Mbosso bado hajaanzisha kampuni ya kusimamia kazi za wasanii.

Leave your comment