Zuchu Afichua Siri Inayoleta Mafanikio Makubwa Kwa Wasanii wa WCB

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

WCB kwa muda mrefu imekuwa mojawapo ya lebo za kurekodi muziki inayotajika zaidi katika tasnia ya muziki ya Tanzania. Lebo hiyo inayomilikiwa na msanii nyota Diamond Platnumz, imeweza kulea na kukuza vipaji vya wasanii ambao kwa sasa wanavuma sana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Bob Junior Aachia ‘Itetemeshe’ Akimshirikisha Lava Lava [Video]

Baadhi ya wasanii ambao wamechipuka kupitia WCB ni Rayvanny, Zuchu, Mbosso, Harmonize, Lava lava na wengine. Kitu kimoja ambacho kimewafanya wasanii wa WCB kuwa na ushawishi mkubwa sana ni ufuasi mkubwa walionao mtandaoni haswaa katika mtandao wa YouTube ambako nyimbo zao huchapishwa.

Mafanikio ya wasanii wa WCB si ya sadfa wala ya kubahatisha, kwani mikakati na taratibu zimeekwa katika lebo hiyo kusudi kuhakikisha kuwa kila msanii anafanya kazi kwa bidii. Zuchu ambaye kwa sasa ni mmoja wa wanamuziki wa kike wanaojivuniaa ufuasi mkubwa, alieleza jinsi wasanii wa WCB hurekodi nyimbo mfululizo bila kupumzika.

Kulingana na Zuchu, wasanii hawa karibu wakati wote wapo studioni wakitengeneza miziki ata baada ya kuachia ngoma zinazovuma katika anga za burudani.

Soma Pia: Remix Tano Kali Zilizoachiwa na Rayvanny

"There is a lot of pressure on my shoulders but uzuri ni kwamba niko kwenye lebo ambayo ndani yake kuna competition. Kwa hivyo unajifunza kukimbizana na timetable. Kabla hata hujaachia nyimbo you already have other songs kwamba ikitakiwa sasa hivi after two weeks ume release another song... tuseme WCB hakuna msanii ambaye atakaa wiki kama haja record wimbo mpya," Zuchu alisema.

Leave your comment