Nyimbo 5 za Kisasa Bongo Zilizochukua Vionjo Kutoka Kwenye Ngoma za Zamani

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wazungu wana kauli yao moja inayosema ‘Old is Gold’ wakimaanisha kuwa vitu vya kale aghalabu huwa na thamani kubwa sana isiyomithilika. Msemo huu unazidi kujidhihirisha kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania kwani wasanii wa kizazi kipya kwa nyakati tofauti tofauti wamekuwa wakirudia kuimba nyimbo zilizotamba zamani au ‘kusample’ midundo ya nyimbo za zamani na kuchukua baadhi ya vionjo na kuweka kwenye nyimbo za sasa hivi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mbili ‘Your Love’ na ‘Tulizana’

Makala hii inaangazia nyimbo tano kutokea kwa wasanii wakubwa hapa Tanzania ambazo zimetumia vionjo, midundo au miondoko ya nyimbo za zamani katika kuundwa kwake:

Wenge - Mimi Mars

Kutokea Mdee Music, Mimi Mars mapema mwaka huu aliachia wimbo wake wa ‘Wenge’. Ukiskiliza kwa makini, wakati Mimi Mars anafungua aya ya pili ya wimbo huu, inaonekana wazi kuwa Mars amechukua vionjo kwenye wimbo wa zamani wa Kilimanjaro band uitwao ‘Tupendane’. Kwenye mahojiano na Lil Ommy, Mars aliweka wazi kuwa ilibidi aombe ruhusa na kuingia mkataba na Kilimanjaro Band kuhusu malipo kabla ya kutoa wimbo huu ambao umeweza kufanya vyema sana.

https://www.youtube.com/watch?v=ZGVxGjGp7Gg

Salome - Diamond Platnumz ft Rayvanny

‘Salome’ iliandikwa na Diamond Platnumz pamoja na Rayvanny lakini vionjo na baadhi ya maneno kwenye wimbo huu yalitokana na wimbo wa zamani wa Saida Karoli uitwao ‘Maria Salome’.  Wimbo huu uliachiwa Septemba 18 mwaka 2016 na ni wimbo uliokosha sana wapenda muziki kutokana na mahadhi yake ya kiafrika . Saida Karoli kwenye mahojiano na Ayo TV alikiri kuwa Diamond Platnumz na Rayvanny waliutendea haki wimbo huo.

https://www.youtube.com/watch?v=_bPjsDcPHks

Tulizana - Mbosso ft Kilimanjaro Band

Kama Mimi Mars kwenye ‘Wenge’, wimbo wa ‘Tulizana’ kutoka kwa Mbosso ni sampuli ya wimbo wa ‘Tupendane’ iliyofanywa na Kilimanjaro band. Mbosso aliamua kwenda mbali zaidi kwa kushirikisha bendi hiyo ya Njenje kwenye wimbo huo ambao ni namba nne kwenye albamu yake ya ‘Definition of Love’.

https://www.youtube.com/watch?v=kP1Awx00FJc

Subalkheri - Nandy & Aslay

Wimbo huu uliotayarishwa na Ema The Boy mara tu baada ya kuachiwa ulipendwa sana na mashabiki lakini kibao hiki kimechukua melody na vionjo vingi kutoka kwenye wimbo wa ‘Subalkheri’ ya Nasma Khamis ambaye alikuwa ni mwanamuziki wa Taarab. Mwaka 2018, Rais wa sasa wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu Rais aliwahi kusema kuwa amevutiwa sana na wimbo huu kutoka kwa Aslay na Nandy.

https://www.youtube.com/watch?v=yIZ9wFdMNl0

Baila – Mri Ben Ali

Wimbo namba 9 kwenye albamu yake Diamond ya ‘A Boy from Tandale’. Kwenye wimbo huu, Ben Ari hajaimba lakini ushiriki wake umetokea kwa yeye kucheza fidla kwenye wimbo. Kando na Diamond Platnumz, Miri ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Grammy tayari alishafanya kazi na wasanii wakubwa duniani kama Jay Z, Alicia Keys pamoja na Janeth Jackson. Ilipofika mwaka 2019 wimbo huu ulishinda tuzo ya Africa Entertainment Awards USA kwenye kipengele cha Best Collaboration.

https://www.youtube.com/watch?v=SVDStt_SlpY

Leave your comment