Rosa Ree Atangaza Kukamilisha Albamu Yake

[Picha: Biggest Kaka]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkali wa muziki wa Hip-hop kutokea nchini Tanzania Rosa Ree ametangaza kuwa amemaliza kuandaa albamu yake. Rosa Ree ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘I'm Not sorry’ Ametangaza kuwa albamu yake imeshakamilika na akawapa zoezi mashabiki wachague jina la albamu hiyo.

"Album done ……. Tuiteje album yetu? Nipe jina la album Anayepatia Jina kali ndo tutakayotumia alafu nampa zawadi," aliandika msanii huyo kwenye ukurasa wake.

Soma pia: Harmonize Afunguka Kuhusu Video Iliyomwonyesha Kajala Akiburudika na Wimbo wa ‘Sandakalawe’

 Rosa Ree aliendelelea kudokeza kuhusiana na albamu yake, Huku akiwaomba kujaribu kutaja wasanii gani ambao watashirikishwa kwenye albamu hiyo. Pia alidokeza kuwa albamu hiyo imeshirikisha wasanii kutokea nchini Tanzania, Kenya pamoja na Uganda.

" Unahisi nimeshirikisha wasanii gani kwenye album yangu? Watag. Hint : Kuna collabo ya Tanzania, Kenya na Uganda,” alisema Rosa  Ree.

Kwa mwaka huu, Rosa Ree ameshatoa nyimbo nne ambazo ni ‘Wote’, ‘Satan’, ‘Its your birthday’ pamoja na ‘I’m not sorry’.

 Kando na Rosa Ree, wasanii wengi kama Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Young Lunya na wako mbioni kutoa albamu.

Soma Pia: S2kizzy: Diamond Ana Zaidi ya Collabo Tatu na Wizkid

Nchini Tanzania, Rosa Ree ni mmoja wa wasanii wakubwa zaidi wanaofanya muziki wa Hip-hop. Yeye ndio msanii wa kike anayejulikana sana kwa kufanya muziko huo.

Leave your comment