Zuchu Amsifia Kidene na Kumkaribisha Kwenye Tamasha la Zuchu Homecoming

[Picha: Kidene Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Zuchu amemtambulisha msanii chipukizi wa Singeli Kidene kama mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza katika tamasha lijalo la Zuchu Homecoming.

Akizungumza kupitia chapisho aliloliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Zuchu alimsifia Kidene kama mwanamuziki mwenye uwezo mkubwa wa kusisimua umati.

Soma piaHarmonize Afunguka Kuhusu Video Iliyomwonyesha Kajala Akiburudika na Wimbo wa ‘Sandakalawe’

Zuchu alikutana na Kidene katika tamasha la Waukae. Kidene alipata fursa ya kupanda jukwaani katika tamasha hilo na kuwaburudisha mashabiki. Umati ulimfurahia na kumshangilia huku Kidene akizidi kuwapa vidonge vya burudani.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii pia wamejitokeza na kumsifia Kidene kwa burudani aliyitoa jukwaani.

Zuchu ni mmoja wa wanamuziki maarufu waliopendezwa na Kidene na kwa sababu hiyo akamtambulisha kama mwanamuziki atakaye kuwa jukwaani katika tamasha lake litakalo fanyika tarehe 21 uwanjani Amani, Zanzibar.

Soma pia: Diamond Platnumz Athibitisha Kufanya Kazi na P Diddy Kutoka Marekani

"Kwa balaa hili lazima awepo Zuchu Homecoming. Tarehe 21/08/2021 uwanja wa Amani Zanzibar . Kwa msanii wa Singeli anaechipukia kwenye show za mtaani kumenoga na mashamsham una kitu kikubwa mimi kama msanii niliesaidiwa na kushikwa mkono lazima nikuunge mkono twende tukaue zenji ..@kidenefighter aisee umebarikiwa mno na balaa lako sio la kawaida wa Zanzibari tunamleta huyu kijana aje aturushe," ujumbe wa Zuchu ulisomeka.

Zuchu amesalia na takriban wiki mmoja kufanikisha tamasha lake la kwanza kama msanii. Tayari ashatoa orodha ya wasanii mashuhuri watakao kuwepo siku hiyo.

Leave your comment