Diamond Platnumz Athibitisha Kufanya Kazi na P Diddy Kutoka Marekani

[Picha: WCB]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Diamond Platnumz amefichua kuwa wakati alikuwa nchini Marekani wiki chache zilizopita, alipata wasaa wa kukutana na rapa mkubwa kutokea nchini humo P Diddy.

Diamond alithibitisha kukutana na msanii huyo kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni lakini kutokana na maelezo ya mwanamuziki huyo, hakutaka kuchapisha chochote kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Soma Pia: S2kizzy: Diamond Ana Zaidi ya Collabo Tatu na Wizkid

"Kweli tulienda kwa Diddy nafikiri siku moja kabla ya uhuru wa Marekani yeah tukakaa kuna vitu tukafanya sema yaliyofanyika yalikuwa sio ya kupost," alizungumza msanii huyo.

Ikumbukwe kuwa msanii P Diddy alihusika sana kwenye maandalizi ya albamu ya ‘Twice As Tall’ kutoka kwa Burna Boy ambayo ilishinda albamu bora ya kimataifa kwenye tuzo za Grammy mapema mwaka huu.

Kikao hicho kinaashiria kuwa kuna uwezekano kuwa P Diddy akahusika kwenye albamu ya Diamond inayotarajiwa hivi karibuni.

Soma Pia: S2kizzy: ‘Tetema’ ya Rayvanny Ndio Wimbo Ulioniletea Mafanikio Zaidi

Kwa siku za hivi karibuni, Diamond Platnumz ameonekana kuwa na ukaribu na wasanii kutokea nchini Marekani kama vile Snoop Dogg, Busta Rhymes, Alicia Keys, Swizz Beatz na wasanii wengine wengi.

Kwa sasa, Diamond Platnumz anatamba na wimbo wake wa Amapiano wa ‘Iyo’ alioshirikisha wasanii kutokea Afrika kusini Focalistic, Mapara A Jazz na Ntoshi Gazzi.

Leave your comment