S2kizzy: ‘Tetema’ ya Rayvanny Ndio Wimbo Ulioniletea Mafanikio Zaidi

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Mganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mtendaji wa Pluto Records S2kizzy amefichua wimbo ambao umemletea yeye mafanikio makubwa sana kwenye muziki kuliko nyimbo zake zote. Akiongea na Sky Walker, S2kizzy alisema kuwa wimbo wa ‘Tetema’ ulioachiwa na Rayvanny na Diamond Platnumz ndio mradi uliofanya vizuri kuliko nyimbo zake zote alizowahi kutayarisha.

"Tetema ilikuwa ni wimbo uliowashirikisha Rayvanny na Diamond ulifanya vizuri sana especially nje na ndani kwa hiyo ulinipa exposure kubwa kwa sababu nlipata deals mbalimbali nje," alidokeza msanii huyo.

Soma Pia: S2kizzy: Diamond Ana Zaidi ya Collabo Tatu na Wizkid

Wimbo wa Tetema uliachiwa Januari 30 mwaka 2019 na bila shaka ulifanya vizuri sana kiasi cha kupata remix kutoka kwa wasanii wakubwa kama Patoranking na Zlatan na ndio wimbo wa Rayvanny uliotazamwa zaidi YouTub.  Kufikia sasa video ya wimbo huo ishatazamwa mara milioni hamsini na nane.

Aidha, S2kizzy pia alizungumzia utayarishaji wa wimbo ya ‘Iyo’ ulioachiwa na Diamond Platnumz na ulio na vionjo vya Amapiano. Akieleza ni  kwa nini waliamua kufanya aina hiyo ya muziki, S2kizzy alisema kuwa "Its African Sound. Zinapofanyika (amapiano) haimaanishi watu wamekosa cha kufanya no ni kwa sababu pia nataka kuchukua soko la sehemu fulani."

Soma Pia: Rayvanny Apata Mafanikio Makubwa na Ngoma Yake Mpya ‘Patati Patata’

"Baada ya sisi kufanya ‘Iyo’ mi nimepata watu South Africa mafans tumeongeza pia South Africa that means hata ufuatiliaji wao kwetu pia umekuwa mkubwa ," alizungumza S2kizzy.

Leave your comment