Rosa Ree Kuwakutanisha Frida Amani, Chemical Ndani ya Ngoma Moja

[Picha: Simulizi na Sauti YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa muziki wa Hip-hop nchini Tanzania Rosa Ree ametangaza ujio wa wimbo mpya ambao utakutanisha wasanii wakike watatu wakubwa wanaofanya vizuri sana kwenye muziki wa Hip-hop hapa Tanzania.

Soma Pia: Rosa Ree Atangaza Kukamilisha Albamu Yake

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Sorry Not Sorry’ kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza kuwa kuna ngoma ipo ambayo inamhusisha yeye, Frida Amani pamoja na Chemical na amewahisi mashabiki kuwa na subira.

"Its about time msikie track moja kati ya Frida Amani Chemical na Goddess! Au mnasemaje?? Mhhh sijui itakuajee …. Stay Tuned iss gon be lit" aliandika rapa huyo kwenye akaunti yake ya Instagram.

Soma Pia: Rosa Ree Awasihi Wasanii wa Bongo Kuacha Kufanya Kiki Katika Muziki

Kwa muda mrefu sasa, wasanii hao watatu wamekuwa wakishindanishwa na wadau wa muziki hapa Tanzania na ujio wa wimbo huo wa pamoja unategemewa kuonesha ushirikiano mkubwa uliopo baina ya wasanii hao.

Mpaka sasa, Rosa Ree hajaweka wazi jina la wimbo huo wala mtayarishaji aliyehusika kuandaa kibao hicho kinachosubiriwa kwa hamu.

Kwa sasa, Rosa Ree anatamba na wimbo wake wa ‘Sorry Not Sorry’, Frida Amani anatamba na wimbo wake wa ‘Imo’ aliomshirikisha msanii Mimi Mars, huku Chemical anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Papara’ uliotoka siku chache zilizopita.

Aidha, Rosa Ree siku chache zilizopita aliahidi kutoa albamu siku za hivi karibuni na msanii huyo alieleza kuwa albamu hiyo itahusisha wasanii wa ndani na nje ya nchi kama Kenya na Uganda. Albamu hiyo itamfanya yeye kuwa msanii wa kwanza wa Hip-hop wa kike nchini Tanzania kutoa albamu.

Leave your comment