Rosa Ree Awasihi Wasanii wa Bongo Kuacha Kufanya Kiki Katika Muziki

[Picha: Rosa Ree Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu Rosa Ree amekosoa wanamuziki wenzake kutoka Tanzania kwa kuzidisha kiki kusudi kuuza muziki wao. Katika chapisho refu alilolieka kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Rosa Ree aliwashauri wanamuziki wa Bongo wazingatie utengenezaji wa muziki mzuri badala ya kiki zisizofaa.

Soma Pia: Wasanii 5 Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Kwenye YouTube Tanzania

Kulingana na Rosa Ree, muziki ni kama bidhaa na mashabiki hutumia bidhaa hiyo kulingana na ubora wake. Alielezea kuwa baadhi ya wanamuziki kutoka Tanzania walikuwa wakitengeneza muziki wa hali ya chini na kuwalazimisha mashabiki wao kuuskiza.

Rosa Ree alisema kuwa kiki zitampa msanii umaarufu kwa muda mfupi kabla ya kumshusha.

Aidha, Rosa Ree alilinganisha tasnia ya muziki wa Tanzania na ile ya nchi zingine kama Nigeria. Alidai kuwa idadi nzuri ya wanamuziki wa Kiafrika kama vile Burna Boy wamefanikiwa bila utata wowote wala kiki.

Rosa Ree pia aligusia suala la wanamuziki kununua watazamaji katika nyimbo zao kwenye mtandao wa YouTube.

Alidai kuwa vitendo kama hivyo sio nzuri kwa taaluma ya mwanamuziki.

"Tunahitaji Kuamka! Wasanii Tuamkeni! I’m so emotional today kwa sababu Nina upendo sanaaaa na wasanii wenzangu pamoja na sanaa yetu kiujumla..... Sanaa yetu imekua ya kiki kiki, u team, kununua views na maswala mengine ambayo hata hayahusu sanaa tena! Msanii kama mwana sanaa na mfanya biashara unatakiwa uzingatie “Product” unayompa “Customer” wako..... mlaji ni shabiki, wewe ni mpishi sasa kwanini umpe mlaji sanaa mavi ikiwa imepakwa asali ( ambayo ni kiki, u team n.k) kwa juu Alafu umlazimishe shabiki ale ulichopakua.... tunaweka focus yetu kwa the wrong things guys Na ndo maana wenzetu wanatuacha nyuma sana! Sijawahi kuskia kiki ya Burna Boy ila sahivi ana grammy na tuzo nyingine nyingi na heshima juu yake!" Rosa Ree aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Leave your comment