Wasanii 5 Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Kwenye YouTube Tanzania

[Picha: Grammy]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Saa chache baada ya kuachia video ya ‘Nikomeshe’ msanii Lavalava kutokea WCB aliweka alama nyingine kwenye muziki wake baada ya kufikisha wafuatiliaji (subscribers) Milioni moja kwenye akaunti yake ya YouTube.

Soma Pia: Diamond Kufanya Collabo na Wiz Khalifa

Kwa miaka ya hivi karibuni, YouTube imekuwa ni mojawapo ya mitandao ambayo wasanii wanategemea sana kuweka kazi zao. Wafuatao ni wanamuziki kutokea nchini Tanzania wanaoongoza kuwa na wafuatiliaji kwenye mtandao huo maarufu duniani:

Diamond Platnumz

Bosi huyu wa WCB alifungua akaunti yake ya YouTube Juni mwaka 2011 na kufikia sasa ana wafuatiliaji takribani Milioni 5 nukta tatu. Hii inamfanya Diamond Platnumz kuwa ndiye msanii mwenye wafuatiliaji wengi zaidi Afrika, chini ya Jangwa la Sahara.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano za Harmonize, Diamond, Zuchu na Alikiba Zinazovuma Tanzania Wiki Hii

Rayvanny

Video zote za Rayvanny zishatazamwa mara Milioni 561 na kufikia sasa amepata wafuatiliaji Milioni mbili nukta tisa kwenye akaunti yake ya YouTube iliyoanzishwa March 2016 kipindi alitambulishwa Wasafi.

Harmonize

Harmonize anawafuatiliaji Milioni mbili nukta sita na idadi hiyo inategemewa kuongezeka pale ambapo ataachia albamu yake ya ‘High School’.

Mbosso

Mbosso Khan pia anaingia kwenye orodha hii akiwa na wafuatiliaji milioni moja nukta sita. Akaunti yake ya YouTube ilianzishwa mwaka 2018 mara tu baada ya kuingia Wasafi. Video ya wimbo wake wa "Hodari" umetazamwa mara Milioni 34 ikiwa ndio video yake iliyotazamwa mara nyingi zaidi kwenye akaunti yake ya YouTube.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Zuchu

Msanii kutokea label ya WCB Zuchu aliweka rekodi ya kufikisha wafuatiliaji milioni moja ndani miezi kumi na moja tangu aanze muziki. Kufikia sasa, ameshafikisha wafuatiliaji Milioni moja nukta tatu kwenye akaunti yake.

Wasanii wengine kutokea nchini Tanzania wenye wafuatiliaji wengi ni pamoja na Alikiba mwenye wafuatiliaji 959,000, akifuatiwa na Nandy mwenye wafuatiliaji 801,000. Wengine ni Aslay na Marioo.

Leave your comment