Nyimbo Mpya: Video Tano za Harmonize, Diamond, Zuchu na Alikiba Zinazovuma Tanzania Wiki Hii

[Picha: Lava lava Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mchuano bado ni mkali kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania kwani kila msanii anajitahidi kutoa wimbo mkali ambao utawafurahisha na kuburudisha mashabiki.

Soma Pia: Busta Rhymes Amsifu Diamond, Amtaja Kuwa Michael Jackson wa Afrika

Ikiwa ni wiki ya kwanza kabisa ya mwezi Julai, zifuatazo ni ngoma 5 ambazo zinatamba sana kwenye mtandao wa YouTube wiki hii:

Soma Pia: Dancer wa Diamond Angel Nyigu Aeleza Walivyotengeza ‘Kamata’ Dance

Nyumba Ndogo – Zuchu

Msanii Zuchu anafungua pazia wiki hii na wimbo wake uliokosha watu wa rika zote ndani na nje ya Tanzania, ‘Nyumba Ndogo’. Kwenye wimbo huu, Zuchu anabadilika kwa kufanya muziki wa singeli akiongeza na vionjo vya mdananda kiasi cha kufanya wimbo huu kuwa maarufu sana nchini Tanzania hasa maeneo ya uswahilini ambapo ndio muziki wa singeli ulipozaliwa.

https://www.youtube.com/watch?v=KsU31FyvFxY

Kamata - Diamond Platnumz

Simba wa Tandale Diamond Platnumz anaendelea kunguruma na wimbo wake wa ‘Kamata’. Video ya wimbo wa ‘Kamata’ mpaka sasa imetazamwa takriban mara milioni tatu nukta mbili kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=0dtdfKEoMuU

Salute - Alikiba ft Rude Boy

Baada ya audio wa wimbo huu kufanya vizuri sana, Alikiba aliamua kutetemesha kiwanda cha muziki nchini Tanzania kwa kuachia video ya Salute iliyotoka rasmi tarehe 30 Juni 2021. Kufikia sasa, video ya Salute imetazamwa takribani mara milioni tatu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=oQ8SycSejrM

Sandakalawe - Harmonize

Harmonize anaendelea kuonesha umaridadi wake kwenye mtandao wa YouTube kupitia video yake ya ‘Sandakalawe’ iliyopata watazamaji wengi ndani ya muda mfupi tu. Kufikia sasa video ya ‘Sandakalawe’ iliyofanyika nchini Nigeria imetazamwa takribani mara milioni nne nukta nne tangu kuachiwa kwake siku tano zilizopita.

https://www.youtube.com/watch?v=JWDTQdQgd4o

Berna Reloaded - Mr Flavour ft Fally Ipupa & Diamond Platnumz

Mr Flavour anaendelea kudhihirisha kuwa muziki mzuri hauna mipaka. Kwenye Berna Reloaded Mr Flavour anawaleta kwa mara nyingine Fally ipupa na Diamond Platnumz. Mpaka sasa, video hii imetazamwa takribani mara milioni mbili na laki saba kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=2LGiIBkg2uw

Leave your comment