Dancer wa Diamond Angel Nyigu Aeleza Walivyotengeza ‘Kamata’ Dance

[Picha: Angel Nyigu Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wimbo mpya wa msanii Diamond Platnumz ‘Kamata’ umepata umaarafu sana nchini Tanzania huku mashabiki wakitengeza densi zao kupitia shindano aliloanzisha Diamond linaloitwa Kamata Dance Challenge.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia Wimbo Mpya ‘Kamata’

Akiongea na chombo kimoja cha habari hapa nchini Tanzania, dancer maarufu wa Wasafi Angel Nyigu ambaye ana takriban wafuasi Milioni 1 kwenye ukurasa wake wa Instagram ameelezea jinsi ambavyo alikuja na wazo la kutengeneza miondoko ya wimbo huo.

"Bosi (Diamond) alikuwa na idea yake, alikuwa na idea ya kitu ambacho anakitaka, so msanii anapokuletea idea yake mimi kama dancer jukumu langu ni kufanya theory iwe practical, so tukatengeneza tulichotengeneza and then akakiona.

Soma Pia: BET Awards: Burna Boy Amshinda Diamond, Aibuka Mshindi wa Best International Act

“Kwa kuwa yeye (Diamond) anajua baadhi ya moves, anajua kitu gani ni kizuri kitu gani ni kibaya akatucorrect, that is how kamata dance move imepatikana," Nyigu alisema.

Nyigu ambaye ameonekana kwenye video nyingi za wasanii wa wasafi kama "Sukari" ya Zuchu na "Jeje" ya Diamond Platnumz pia aliongeza kuwa ilichukua takriban siku mbili hadi tatu kujifunza miondoko ya wimbo huo.

"Ilichukua almost two days ama three days, kama siku tatu hivi tulipractise and thats how kamata dance came to be," Nyigu alieleza.

Sambamba na hilo pia, HBajuni ambaye pia ni dancer wa WCB alieleza kuwa miondoko ya wimbo wa ‘Kamata’ zilitengenezwa na yeye Bajuni, Angel Nyigu, Baby Drama, Mose Iyobo na Diamond Platnumz.

Bajuni ambaye amepata umaarufu mkubwa baada ya Diamond Platnumz kumtaja kwenye wimbo wake wa ‘Waah’ alinena "Tulihangaika kutufata style tulikuwa ni mimi, kuna dancer anaitwa Angel Nyigu, Baby Drama kuna Diamond mwenyewe na Mose Iyobo hao ndo tulikuwa baze kutafuta hiyo style."

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha The Switch, Bajuni pia alimuweka wazi dancer ambae alikuwa anaonekana anacheza huku maneno yakiwa yanapita kwenye audio ya wimbo wa kamata. Bajuni alisema kwamba dancer Yule anaitwa Baby Drama na Diamond ndiye aliyeamua yeye kuonekana kwenye video ile ambayo mpaka sasa imeshatazmwa mara milioni moja na laki nne kwenye mtandao wa YouTube.

"Yule dancer anaitwa Baby drama na kumchagua alimchagua yeye mwenyewe (Diamond). Sikujua sababu ni nini, unajua Naseeb (Diamond) ni mtu ambaye anajua kipi kibaya kipi kizuri na siku zote ni mtu ambae anapenda vitu vizuri, yani vitu perfect," alisema dancer huyo ambaye ameonekana kwenye video nyingi za Diamond Platnumz.

Leave your comment