Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia Wimbo Mpya ‘Kamata’

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki na bosi kutokea label ya WCB Diamond Platnumz ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Kamata’.

‘Kamata’ umetayarishwa na Salmin Kasimu Maengo almaarufu kama S2kizzy ambaye ameshafanya nyimbo kadhaa na Diamond Platnumz kama vile; ‘Kanyaga’, ‘Far Away’ pamoja na ‘Baba Lao’.

Soma Pia: S2kizzy Azungumzia Ujio wa Albamu Mpya ya Diamond Platnumz

‘Kamata’ ni wimbo wa bongo fleva wenye vionjo vya Afropop. Wimbo huo unategemewa kukita sana katika kumbi na club mbalimbali hapa Afrika Mashariki.

Kwenye wimbo huu, Diamond platnumz anaonekana kumsifia mtoto wa kike anayecheza nae, kwenye wimbo na kumuelekeza kwa vitendo wapi ashike ili azidi kumpagawisha.

Kwenye verse ya kwanza, Diamond Platnumz anaghani "Kamata Kiuno, Kamata bega, kamata kichwa ka ndoo na bega" huku kwenye kiitikio akirudia kumwambia mpenzi wake akamate ili wacheze vizuri.

Soma Pia: Diamond Ashutumu Forbes kwa Kudharau Tasnia ya Muziki ya Tanzania

Ndani ya dakika 30 tu wimbo huo ulikuwa umeangaliwa takriban mara 30,000 huko YouTube huku likes zikiwa takribani 3,600 ndani ya muda huo mfupi.

‘Kamata’ ni muendelezo wa Diamond Platnumz kupendelea kutoa nyimbo zake mwezi Juni ambapo mwaka 2019 siku kama ya leo ya tarehe 25 alitoa ‘Kanyaga’, mwaka 2018 tarehe 9 Juni alitoa video ya wimbo wa ‘Inama’ aliofanya na Fally Ipupa pia 2017 tarehe 21 Juni alitoa wimbo wa ‘Fire’ aliofanya na Tiwa Savage kutokea nchini Nigeria.

Ikumbukwe pia wimbo wa ‘Kamata’ umetoka siku mbili kabla ya hafla ya utoaji wa tuzo za BET zinazotarajiwa kufanyika Jumapili ya tarehe 27 mwezi huu.

https://www.youtube.com/watch?v=IkHwdjWHs50

Leave your comment