Diamond Ashutumu Forbes kwa Kudharau Tasnia ya Muziki ya Tanzania

[Picha: Buzz Central]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Diamond Platnumz ameishutumu kampuni ya Forbes kwa kuwadharau wanamuziki wa Tanzania. Akizungumza wakati wa mahojiano ya hivi karibuni, Diamond alidai kuwa kampuni hiyo ilivunja heshima ya tasnia ya burudani ya Tanzania katika orodha yake ya wasanii tajiri Afrika.

Hapo awali, Diamond aliibua malalamiko baada ya kuorodheshwa chini kati ya wasanii tajiri barani Afrika. Wanamuziki wengi waliochukua nafasi ya kwanza kwenye orodha hiyo walikuwa kutoka Afrika Magharibi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya : Zuchu Aachia ‘Nyumba Ndogo’, Ngoma Mpya ya Singeli

Katika mahojiano hayo, Diamond alidai kuwa tasnia ya burudani ya Tanzania imekuwa ikidharauliwa na kuongeza kuwa haikuhusu yeye kama mwanamuziki binafsi bali tasnia yote ya muziki ya kitanzania.

Alieleza kuwa kulikuwa na dhana potofu kwamba wanamuziki kutoka Tanzania sio matajiri.

Kulingana na Diamond, wasanii wa Tanzania wamepanda kwa kiwango cha kimataifa na hawapaswi kudharauliwa vile.

Soma Pia: Diamond Platnumz Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Hivi Karibuni

"Unajua mimi sitazami vitu hizo kwenye upande wa mimi kama Diamond. Naitazama kama kuivunjia heshima Swahili Nation. Yaani huwezi kuwa wasanii ni Kiswahili kama wewe ni mbumbumbu. Kwa hivyo  siwezi kubali kuona kwamba kuna mtu anatia dosari ama kudhalilisha jamii ya Kiswahili. Siwezi kukubali," Diamond alisema.

Hapo awali, baadhi ya watanzania kwenye mitandao ya kijamii walikuwa wameandamana kupinga orodha hiyo wakisema kwamba ilikuwa ya upendeleo.

Leave your comment