BET Awards: Burna Boy Amshinda Diamond, Aibuka Mshindi wa Best International Act

[Picha: Diamond Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tuzo za BET zilifanyika usiku wa kuamkia tarehe 28 Juni na msanii Burna Boy kutokea nchini Nigeria amechukua tuzo hiyo kwenye kipengele cha msanii bora wa kimataifa (Best International Act) kipengele ambacho aliwekwa kuwania na nyota wa Afrika Mashariki Diamond Platnumz.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia Wimbo Mpya ‘Kamata’

Diamond Platnumz alihudhuria hafla ya tuzo hizo zilizofanyika Microsoft theatre, Los Angeles huko California Marekani akiwa amevalia vazi la kimasai na kusababisha kuteka hisia za watu wengi kwenye zulia jekundu.

Hii ni mara ya tatu kwa Diamond Platnumz kukosa tuzo ya BET kwani alishiriki 2014 akapotza kwa msani Davido kutokea nchini Nigeria, pia alishiriki mwaka 2016 ambapo msanii Black Coffee kutokea Afrika kusini alichukua tuzo hiyo na mwaka huu pia, msanii Burna Boy kutokea Nigeria anachukua tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo kuanzia 2019 hadi sasa.

Soma Pia: S2kizzy Azungumzia Ujio wa Albamu Mpya ya Diamond Platnumz

Kabla ya kuhudhuria tuzo hizo wadau mbalimbali wa burudani na wasanii kutokea nchini Tanzania kama Shilole, Shetta, Zuchu, Lavalava, Queen Darleen, Jux, Baba Levo na wengineo waliandika jumbe mbalimbali kumtakia heri Diamond Platnumz kwenye tuzo hizo ambazo husheherekea mafanikio ya wasanii weusi nchini marekani.

Licha ya kukosa tuzo hiyo, Diamond Platnumz anaweka rekodi ya kuwa msanii kutokea Afrika Mashariki anayeongoza kushiriki kwenye tuzo za BET.

Mara baada ya hafla hiyo kuisha, Diamond Platnumz kupitia akaunti yake ya Instagram aliandika akiwashukuru mashabiki zake kwa kumsapoti muda wote na akaongeza pia anategemea kwamba watanzania watampa ushirikiano msanii mwingine atakayeshiriki kwenye tuzo kama ambavyo yeye amepata.

“kupitia tuzo hii nimeona ni kiasi gani watanzania tuna umoja, upendo na kuthamini vya kwetu...Nawashukuru sana kila mmoja wenu kwa upendo mkubwa mlionionesha...Nifaraja kuona Dunia inapotaja nchi zenye wanamuziki bora Tanzania inatajwa, ni jambo la kumshukuru Mungu....Na naamini wakati mwingine Tutaibeba...,” aliposti Diamond.

Leave your comment