Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

[Picha: Lava lava Instagram]

Mwandishi: Charles maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ikiwa imetimia wiki ya kwanza tangu mwezi Julai uanze wanamuziki kutokea nchini Tanzania wamekataa kuchukua likizo kwa kuendelea kuporomosha na kuachia nyimbo nzuri ambazo zitaburudisha mashabiki na wapenzi wa muziki.

Soma Pia: Rayvanny Kumtambulisha Msanii wake wa Kwanza Hivi Karibuni

Bila shaka Julai imeanza na nyimbo nzuri sana na zifuatazo ni nyimbo mpya zilizotoka wiki hii:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia Video Rasmi ya 'Nyumba Ndogo'

Hawakatai - Ney wa Mitego

Kwenye wimbo huu, Nay wa Mitego anaeleza jinsi ambavyo wadada wenye tamaa ya pesa wanavyorubuniwa kirahisi na wanaume wenye magari, pesa na vitu vya thamani. Kufikia sasa wimbo huo umetazamwa takriban mara Laki moja na ishirini na tano elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=fNakH7INftw

Mpunguze - Tunda Man ft Young Lunya

Baada ya kufanya vizuri na video ya wimbo wake wa ‘True Love’, Tunda man ameamua kuunganisha nguvu na rapa Young Lunya kwenye ngoma mpya ya ‘Mpunguze’. Kwenye wimbo huu, Tunda man anatoa wito kwa mashabiki zake kuwa waache kushikilia marafiki wasiokuwa na manufaa na wenye tabia zisizopendeza.

https://www.youtube.com/watch?v=9T-jzI5mt3o

Country Wizzy - Hip hop

"Na siku hizi dili zangu mi ni doladola, huwezi kunikuta kwenye daladala" huo ni mojawapo kati ya mstari uliopo kwenye mdundo huu mpya wa Country Boy uliotoka Julai 4 mwaka 2021 na kutayarishwa na Bboy Beats. Kwenye wimbo huu Country Wizzy ambaye yuko chini ya Konde Music anatamba kwa kuonesha ni kiasi gani muziki wa Hip-hop upo juu na ni raha kiasi gani anajisikia kuutumikia muziki wa Hip-hop.

https://www.youtube.com/watch?v=96_LYI-MqrE

Kwa Kalvari - Walter Chilambo

Baada ya kutamba na remix ya wimbo wa ‘El Shadai, Walter Chilambo ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Love Music Brand anarudi kwa nguvu na ‘Kwa Kalvari’ Wimbo huu unaonesha ni jinsi gani rehema na neema za Mungu zinavyowakirimu wanadamu. Huu ni wimbo uliojaa hisia na ni zawadi kwa wapenda muziki wa Injili.

https://www.youtube.com/watch?v=aZwXhjRPZIs

Nikomeshe – Lava lava

Kwenye wimbo huu, Lava lava anaelezea jinsi mapenzi yanavyomtesa na kumfanya apate sonona baada ya kukimbiwa na mpenzi wake aliyekuwa anampenda sana. Wimbo huu mpaka sasa umetazamwa takriban mara 270,000 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=m0fEkdKfh3c

Leave your comment

Top stories

More News