Rayvanny Kumtambulisha Msanii wake wa Kwanza Hivi Karibuni

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Rayvanny ametangaza kuwa hivi karibuni atamtambulisha msanii wa kwanza ambaye amemsaini chini ya lebo yake ya Next Level Music.

Rayvanny akizungumza baada ya kumkaribisha mwimbaji wa Nigeria Guchi nchini Tanzania, alidai kuwa maandalizi yote ya uzinduzi wa msanii huyo yamekamilika.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Mpya Zilioachiwa na Diamond, Rayvanny, Harmonize na Alikiba Wiki Hii

Alieleza kuwa utengenezaji wa nyimbo za kwanza za msanii huyo zimekamilika. Kwa sasa Rayvanny amesema kuwa timu yake ya Next Level Music  inashughulikia utaratibu wa kumtambulisha mwanamuziki wa kwanza kutoka lebo hio.

Rayvanny pia aliwaomba mashabiki wake kuunga mkono lebo yake na msanii ambaye atamtambulisha hivi karibuni.

"Kwa Next Level kila kitu kipo tayari, tume shoot videos tofauti tofauti. Lakini pia tumejipanga in short na msanii yuko tayari . So its just the plan na tunamtoa, lakini nafikiri kwamba watu wamesubiri muda mrefu. Kwa sababu mimi sikutaka nikurupuke nitoe tu msanii. Kwa sababu ningetaka nigemtoa ata ile siku ya kwanza,"Rayvanny alisema.

Soma Pia: Rayvanny Amtetea Diamond Platnumz Baada ya Kukosa Tuzo la BET

Baada ya kufungua lebo yake ya Next Level Music, Rayvanny alikuwa msanii wa pili kutoka lebo ya WCB kuanzisha lebo yake ya kurekodi. Harmonize ambaye ni msanii wa zamani wa lebo hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz alianza lebo yake iliyopewa jina la Konde Worldwide Music.

Tofauti ya lebo yake Harmonize na Rayvanny ni kuwa Rayvanny bado yuko chin ya WCB, ilhali Harmonze alijitoa kabisa.

Leave your comment

Top stories