Rayvanny Amtetea Diamond Platnumz Baada ya Kukosa Tuzo la BET

[Picha: All Africa]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika Tanzania Rayvanny amemtetea Diamond Platnumz siku chache baada ya kushindwa kwenye tuzo za BET. Diamond alikuwa ameteuliwa katika kitengo cha Best International Act pamoja na wanamuziki wengine wa Kiafrika akiwemo Burna Boy na Wizkid.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia Video Rasmi ya 'Nyumba Ndogo'

Burna Boy alishinda tuzo hiyo. Diamond kukosa tuzo hiyo iliibua maoni tofauti kati ya wadau mbali mbali katika tasnia ya muziki. Mashabiki wengi hata hivyo walimpongeza Diamond kwa kufikia kiwango cha uteuzi wa tuzo hizo.

Kulingana na Rayvanny, uteuzi pekee ulimtosha Diamond na haikuwa lazima kwake kushinda. Alisema kuwa kushindwa huko hakumaanishi kuwa Diamond sio mwanamuziki mzuri.

Rayvanny aliendelea kwa kutoa mifano ya wanamuziki wengine wakubwa wa Kiafrika kama vile Davido ambaye alikosa uteuzi. Rayvanny anaamini kuwa ni bora mwanamuziki apoteze kwenye tuzo ili aweze kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Mpya Zilioachiwa na Diamond, Rayvanny, Harmonize na Alikiba Wiki Hii

"Mashindano kushiriki tu wenyewe wanasema wewe ni mshindi. Kwa sababu mpaka ushiriki ina maanisha watu wamekuzingatia. Davido hajakuwepo hata kwenye nomination, kwa hivyo wao walimpick kwa kuona kuwa ali deserve kuweko pale. Lakini ku deserve kuwekwa pale hakumaanishi kuwa utashinda. Kushinda na kushindwa yote ni matokeo. Lakini what I belive ni mara nyingi ni bora ushindwe ili uongeze nguvu pia," Rayvanny alieleza.

Kwa sasa, Diamond yuko Marekani ambapo anafanya kazi kwa kushirikiana na wanamuziki wa Marekani kwenye albamu yake.

Leave your comment