Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia Video Rasmi ya 'Nyumba Ndogo'

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutoka lebo ya WCB Zuchu ameachia video rasmi ya wimbo wake mpya ‘Nyumba Ndogo’.

Video ya ‘Nyumba Ndogo’ ni yenye maudhui ya densi na inaambatana na mistari ya wimbo huo, kwani Zuchu anaonekana akikorofishana na mke mwenza.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Mpya Zilioachiwa na Diamond, Rayvanny, Harmonize na Alikiba Wiki Hii

Video hio imepokelewa vizuri na inazaidi ya watazamaji laki tatu masaa manane baaday ya kuachiwa.

Kanda hii inakuja siku kadhaa baada ya Zuchu video ya ‘Nyumba Ndogo’ densi ambao kwa sasa una zaidi ya watazamaji milioni tatu kwenye YouTube.

‘Nyumba Ndogo’ ni ngoma aina ya Singeli. Wimbo huu unazungumzia kisa cha mwanamke ambaye bwanake ameoa bibi wa pili.

Soma Pia: Ray C Awasihi Watanzania Kuwaunga Mkono Wasanii wa Bongo

Kwenye wimbo huu, Zuchu anachukua nafasi ya ‘Nyumba Ndogo’  kwa jina lingine ‘Mwanamke wa Pili’.

Anaeleza kuwa bwanake amekuwa akilalamika kwamba bibi yake wa kwanza hajawajibika hasa katika kuanda chakula na kumlinda yeye kama mumeo.

“Yamenifika kwa koo! We mwanamke mwenzangu…Bwana ako analalamika kila akija nyumbani, eti hujui kupika, kula kwako hatamani, kwangu lakipenda tembele toto laini laini… Nimemganda mumeo kama kichwa na kisogo…,” Zuchu aliimba.

Wimbo huu umetengezwa na DJ Kidogodogo, huku matayarisho ya mwisho yakifanywa na Lizer.

https://www.youtube.com/watch?v=KsU31FyvFxY

Leave your comment