Nyimbo Mpya: Ngoma Mpya Zilioachiwa na Diamond, Rayvanny, Harmonize na Alikiba Wiki Hii

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Soko la bongo fleva linazidi kukua na hii inasababishwa na ukweli kwamba wasanii wanatoa ngoma nyingi na nzuri ambazo huvutia mashabiki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

Wiki hii mambo yamekuwa sukari sana kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania baada ya wasaniii wakubwa kama Diamond Platnumz, Harmonize, Moni Centrozone, Alikiba na wengine wengi kuachia nyimbo, ilikuwa ni kazi ya shabiki tu kuchagua aanze kusikiliza bidhaa ya msanii gani ili afurahi.

Soma Pia: Barakah The Prince Adai Wimbo Wake ‘Yanachosha’ Ndio Ngoma Mpya Bora Zaidi Bongo

Hizi ni nyimbo mpya tano ambazo zimetoka na zimefanya vizuri sana wiki hii:

Kamata - Diamond Platnumz

Baada ya ukimya wa miezi saba, tarehe 25 Juni msanii Diamond Platnumz aliamua kuachia wimbo wake wa kwanza mwaka huu uitwao ‘Kamata’. Wimbo wa ‘Kamata’ ni mchanganyiko wa Afro-pop pamoja na bongo fleva.

https://www.youtube.com/watch?v=0dtdfKEoMuU

Sandakalawe - Harmonize

Huu ni wimbo wa Harmonize almaarufu Konde Boy. Sandakalwe ni wimbo wenye vionjo vya Amapiano na kupitia wimbo huu Harmonize ameonesha kuwa yeye anaweza kubadilika kwa kuimba mitindo tofauti tofauti ya muziki. Kwa sasa wimbo huu haupatikani YouTube kwa kuwa umetolewa baada ya ya mamalishi kuhusu hatimiliki na Kampuni ya Empire.

Kiss Me - Bahati ft Rayvanny

Kwa mara nyingine msanii Bahati kutokea Kenya anaungana na Rayvanny kutuletea ngoma kali sana. Wimbo huu wa ‘Kiss Me’ ni mojawapo ya nyimbo kwenye albamu yake Bahati yenye jina ‘Love Like This’. Masaa saba tangu kuachiwa, ngoma hii ina zaidi ya watzamaji laki mbili.

https://www.youtube.com/watch?v=RM2GGAtvn9g

My Life - Moni Centrozone ft Jux

Huu ni wimbo wa kwanza wa Moni Centrozone tangu aingie rasmi kwenye mkataba na kampuni ya kusimamia kazi za wasanii Rooftop entertainment. Kwenye wimbo huu Moni anaelezea maisha yake ya "kuhustle" yalivyokuwa tangu anaanza muziki mpaka sasa.

https://www.youtube.com/watch?v=akyk7aeolqU

Salute - Alikiba ft Rudeboy

Wimbo ulitoka Juni 24 mwaka huu ambapo Alikiba alishirikiana Rudeboy kutoka Nigeria. Katika wimbo huu, Alikiba anampa asante mpenzi wake ambaye alikuwa nae kwenye shida na sasa anamwambia shukran kwa kuweza kumvumilia.

https://www.youtube.com/watch?v=XOsaB1HbB6s

Leave your comment