Barakah The Prince Adai Wimbo Wake ‘Yanachosha’ Ndio Ngoma Mpya Bora Zaidi Bongo

[Picha: Barakah The Prince Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Bongo Barakah The Prince ameibuka na kukosoa wasanii wenzake kwa kutengeneza muziki aliyoitaja kuwa ya hali duni.

Katika taarifa ambayo alichapisha kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Barakah The Prince alidai kuwa hajaona wimbo wowote kutoka kwa mwanamuziki wa Bongo ambao ni bora kuliko wimbo wake wa hivi karibuni uliopewa jina la ‘Yanachosha’.

Soma Pia: Dancer wa Diamond Angel Nyigu Aeleza Walivyotengeza ‘Kamata’ Dance

 Kulingana na Barakah The Prince, wanamuziki wengi wa Kitanzania wametoa ngoma zao lakini hakuna inayofikia ‘Yanachosha’.

Barakah The Prince aliwashauri wenzake katika tasnia ya burudani ya Tanzania kufanya kazi kwa bidii, akiongeza kuwa wale ambao watafanya kazi nzuri watatambuliwa kwa kazi zao.

"Daaah Kiukweli Mpaka Sasa Sijaona Wimbo Mzuri Umetoka Kama Huu Yanachosha. Japo wapo Wengine Wametoa Nyimbo Kali..Ila Hao wasanii wenu Mnaowapigia Mayowe mob Trust Me Hamna Kitu Wamefanya, Na Wanaifanya Hii Game kwa mazoea sana Na Ninyi Mashabiki Mnazidi Kuharibu kwa kuwapa Kichwa Na huo Ukubwa Bandia Aisee.

Read Also: Watu 7 Mashuhuri Waliompongeza Diamond Licha ya Kukosa Tuzo la BET

“Wasanii Wakali kazeni Huu Mziki sasa Upo Wazi Kazi Nzuri Itatembea tu hata kwa mwendo wa kobe. Naenjoy Sana napoona watu wanatoa nyimbo," aliandika Barakah the Prince.

Taarifa hiyo ilivutia maoni tofauti kutoka kwa mashabiki na wadau wengine katika tasnia ya burudani Tanzania.

Ni muhimu kutaja kuwa wasanii wa Bongo sikuhizi hutumia mbinu tofauti kusukuma kazi zao, na huenda Barakah the Prince anatumia ujumbe huo kama kiki ili kuwafanya watu kutazama ngoma yake mpya.

https://www.youtube.com/watch?v=q-G334cQfR4

Leave your comment