Watu 7 Mashuhuri Waliompongeza Diamond Licha ya Kukosa Tuzo la BET

[Picha: Diamond Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tuzo za BET zilifanyika usiku wa kuamkia tarehe 28 na habari kubwa iliyopo kwa sasa nchini Tanzania ni suala la Diamond Platnumz kukosa tuzo hiyo ambayo watanzania wengi walikuwa wameipania sana.

Licha ya Diamond Platnumz kukosa tuzo hiyo, watu wengi mashuhuri wameonekana kumpa pongezi staa huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa "Kamata".

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia Wimbo Mpya ‘Kamata’

Wafuatao ni watu 10 mashuhuri ambao wametumia mitandao yao ya kijamii kumpatia pongezi Diamond Platnumz.

Baba Levo

Baba levo aliandika: “Nchi nzima inakutambua kama Shujaa wetu Diamond Platnumz usirudi nyuma vita bado inaendelea.”

Gigy Money

Msanii Gift Stanford almaarufu kama Gigy Money alimpongeza Diamond akisema “Tuanze na Stage aliyofikia boss wangu. Aliweza kumfanya Rayvanny kuwa msanii wa kwanza East Africa kuchukua tuzo ya BET na kwa hilo basi atabaki kuwa mshindi."

Soma Pia: BET Awards: Burna Boy Amshinda Diamond, Aibuka Mshindi wa Best International Act

Innocent Bashungwa

Viongozi wa serikali nao hawakuwa nyuma kutoa pongezi zao. Waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa sio tu kwamba alimpongeza Diamond kwa kutajwa kwenye tuzo hizo pia alimpa heko Diamond kwa kuvaa vazi la kimasai kwenye hafla hiyo

"Umeitangaza nchi yetu, umetangaza sanaa ya muziki wa Tanzania. Umetangaza utamaduni wetu kupitia vazi maridadi la kimasai," aliandika Bashungwa.

Khadija Kopa

Mwanamuziki wa Taarab Khadija Kopa ambae ana ukaribu mkubwa na Diamond Platnumz aliandika: "Hujashindwa baba, wewe ni mshindi kutajwa jina lako kwenye zile tuzo ni heshima kubwa sana usikate tamaa"

Mkubwa Fella

Mkubwa Fella ambaye ni mojawapo wa wasimamizi wa Diamond Platnumz pia alimpongeza Diamond na kumuhasa apeleke juhudi zake kwenye kutengeneza albamu yake. Kupitia Instagram akaunti yake Mkubwa Fella aliandika: "Hongera mwanangu muhimu ulipofika ni Ndoto yetu, Inshaallah Mungu ana mipango yake sisi tuendelee kuipenda nchi. Sasa naomba tuendelee na kazi za albam.”

Bahati

Mwanamuziki kutokea Kenya Bahati pia hakuwa nyuma kumpongeza Diamond Platnumz kwa ushiriki wake kwenye tuzo hizo na pia alitumia chapisho hilo la Twitter kumkumbusha Diamond kuna vijana wengi wanamuangalia yeye kama kioo hivyo asikate tamaa.

“Kakangu mkubwa!!! @diamondplatnumz wewe bado ni mshindi. You have achieved a lot in your young age bro and let no one lie to you... you inspire a lot of kids in the Swahili nation & beyond! You inspire them to know you can come from nothing to something; zero to hero.”

Gerson Msigwa

Gerson Msigwa ambaye ni msemaji mkuu wa serikali pia alimpongeza Diamond Platnumz kwa hatua aliyofikia na kuahidi kuwa tuzo hiyo itarudi nyumbani muda ukiwadia. Kupitia akaunti ya Twitter Gerson aliandika : "Hatukupata tuzo lakini tumeongeza heshima. Kudos @diamondplatnumz Watanzania tunajua wewe ni Mshindi, Mpambanaji, Mzalendo wa kweli na Mwanamuziki bora sana Afrika na Duniani. Tutaipata wakati mwingine.”

Leave your comment