Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

[Picha: DJ Mwanga]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mambo yanaendelea kupamba moto kwenye kiwanda cha Bongo Fleva kwani nyimbo mpya na nzuri zinazidi kutoka kila kukicha Hivyo basi, makala hii ni makhususi kabisa kwa ajili ya kuonesha ni nyimbo gani ambazo watanzania wanazisikiliza sana kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Moni Centrozone Aeleza Sababu ya Kuandika Wimbo Wake ‘My Life’

Zifuatazo ni nyimbo tano ambazo zinazovuma sana kwenye mtandao wa YouTube wiki hii:

Nyumba Ndogo - Zuchu

Zuchu anashika namba moja na wimbo wake wa Nyumba Ndogo. Wimbo huo umetazamwa mara Milioni mbili nukta nane. Hii ni mara ya kwanza kwa msanii Zuchu kuimba singeli ila mashabiki wameonekana kupenda na kufurahia ujio mpya wa msanii huyo.

https://www.youtube.com/watch?v=dm-nmRCUiHM

Bena Reloaded- Mr Flavour ft Fally Ipupa & Diamond Platnumz

Kutokea kwenye label ya 2nite entertainment, Mr Flavour anawaunganisha tena Diamond Platnumz na Fally Ipupa kwenye ya wimbo huu ambao mpaka sasa umetazamwa mara milioni mbili nukta nne. Wimbo huu ni remix ambapo kwenye toleo la kwanza la wimbo huu alikuwepo Fally Ipupa lakini kwenye remix akaingia Diamond Platnumz.

https://www.youtube.com/watch?v=2LGiIBkg2uw

Kamata - Diamond Platnumz

Baada ya ukimya wa miezi saba, tarehe 25 Juni msanii Diamond Platnumz aliamua kuachia wimbo wake wa kwanza mwaka huu uitwao ‘Kamata’. Wimbo wa ‘Kamata’ ni mchanganyiko wa Afro-pop pamoja na bongo fleva.

Soma Pia: Dancer wa Diamond Angel Nyigu Aeleza Walivyotengeza ‘Kamata’ Dance

https://www.youtube.com/watch?v=0dtdfKEoMuU

Ndombolo - Kings Music

Wimbo huu wa kuchezeka umeunganisha vichwa vinne kutokea Kings Music yaani Alikiba, Abdu Kiba, K2ga na Tommy Flavour. Mpaka sasa wimbo huo umetazamwa zaidi ya mara milioni tatu kwenye mtandao YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=Cf-5DuXPMzY

Salute - Alikiba ft Rudeboy

Wimbo ulitoka Juni 24 mwaka huu ambapo Alikiba alishirikiana Rudeboy kutoka Nigeria. Katika wimbo huu, Alikiba anampa asante mpenzi wake ambaye alikuwa nae kwenye shida na sasa anamwambia shukran kwa kuweza kumvumilia.

https://www.youtube.com/watch?v=XOsaB1HbB6s

Leave your comment