Moni Centrozone Aeleza Sababu ya Kuandika Wimbo Wake ‘My Life’

[Picha: Clouds Media TZ]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Moni Centrozone ameeleza ni nini kilichompelekea kuandika wimbo wake mpya unaofanya vizuri uitwao ‘My Life’ akimshirikisha Jux.

Soma Pia: Moni Centrozone Ajiunga na Rooftop Entertainment

Moni ambaye ana wafuasi laki tano kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa kwenye mahojiano kwenye kipindi cha Empire alisema wimbo huo unaonesha harakati zake za kimuziki kwa ujumla na namna ambavyo alikwepa vitu hasi kwenye maisha yake kama pombe, madawa na magonjwa.

"Nilikuwa niko na RosaRee nikawa namsikilizisha hii nyimbo ikafika ile sehemu ya. …….. sometimes mlo mmoja mama anauzia bagia, akastopisha (Rosa Ree) akaniambia daa Moni mama angu alikuwa anauza bagia shuleni. Hadi goose bumps zimemtoka ikabidi arudie tena tulikuwa tupo kwenye tour bus," Moni alisema.

Soma Pia: Barakah The Prince Adai Wimbo Wake ‘Yanachosha’ Ndio Ngoma Mpya Bora Zaidi Bongo

Moni ambaye sasa yuko kwenye label ya Rooftop Entertainment alitumia mahojiano hayo pia kuwahasa wasanii wadogo walioko mikoani waje Dar es salaam maana muziki upo Dar es salaam. Aliwatolea mfano wanamuziki Dwini na Gifted waliotoka Dodoma kuhamia Dar es salaam ili kufanya muziki.

Moni ambaye amekulia na kulelewa majengo sokoni huko Dodoma alisema "Kiukweli gemu ipo Dsm kwa mkoani naona watu wanastruggle sana kuweza kusikika. Lazima uje huku ( Dar es salaam) kwa sababu wimbo unaweza kufanya vizuri ukahitajika kwenye interview uweze kusambaza nyimbo, lazima uwe huku," alisema Moni.

Moni aliweka wazi pia kwamba hapendelei kuitwa msanii wa Trap na anapendelea sana kuitwa msanii wa Hip-hop kwani yeye anafanya hip-hop kwa ujumla sio muziki wa trap peke yake. Kwa sasa Moni anatamba na wimbo wake uitwao "My Life" akimshirikisha Jux, video ya wimbo huo mpaka sasa imetazamwa takriban mara 45,000 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=AbJJmkjsSe4

Leave your comment