Ujumbe wa Zuchu Kwa Mashabiki Baada ya Tamasha Lake Kupata Mafanikio

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutokea lebo ya WCB Zuchu amechapisha ujumbe wa shukrani kwa mashabiki wake kwenye ukurasa wa Instagram. Zuchu alituma ujumbe huo baada ya tamasha lake la Zuchu Homecoming lililofanyika wikendi kupata mafanikio makubwa.

Soma Pia: Zuchu Apigiwa Simu na Rais Samia Akiwa Katikati ya Tamasha lake la Zuchu Homecoming [Video]

 amasha hilo lilikuwa na umuhimu kubwa kwa Zuchu kwani lilikuwa tamasha lake la kwanza kama mwanamuziki tangu aingie kwenye tasnia ya muziki takriban mwaka mmoja uliopita. Kwenye chapisho lake mtandaoni, Zuchu aliwashukuru mashabiki wake kwa kujitokeza na kumuunga mkono.

Aidha, alisema mategemeo yake kuhusu mafanikio ya tamasha hilo yalikuwa yameridhishwa. Kulingana na Zuchu, tamasha lake lipo miongoni mwa matamasha yaliyo kwenye historia kwa kuwa na watu wengi sana waliohudhuria.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia ‘Yalaaaa’

"Naomba nianze na kuwashukuru Wazanzibari wenzangu na mashabiki zangu wote kwa ujumla .Jana Mlijaa Sana Nawapenda mno Kwa hili mmeniunga mkono Kwa zaidi nilivyotegemea .Tumevunja history ya show iliyojaza zaidi Zanzibar," Zuchu aliandika.

Aliendelea kwa kuwashukuru wasanii wenzake waliojitokeza na kumuunga mkono kwenye tamsaha hilo. Zuchu hata hivyo aliomba radhi kwa wasanii kwa ugumu wowote ambao walikumbana nao katika tamasha lake.

"Lakini naomba niwashukuru wasanii wenzangu kwa support yenu naomba sana pia niombe samahani kama kuna mapungufu yoyote yalijitokeza," chapisho la Zuchu lilisomeka.

Zuchu amepongezwa na wadau mbali mbali katika tasnia ya muziki ya Tanzania kutokana na mafanikio ambayo tamasha lake lilipata.

Leave your comment