Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo na Wasanii Diamond, Rayvanny, Zuchu na Ibraah

[Picha: Ghafla Twitter]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kiwanda cha muziki nchini Tanzania kimeendelea kuwa hai kwani wanamuziki tofauti tofauti wameedelea kutoa nyimbo kali. Kwa wiki hii wasanii kama Diamond Platnumz, Ibraah, Zuchu na wengineo wameendelea kupamba kiwanda cha Bongo Fleva kwa nyimbo nzuri.  Nakala hii imelenga kuangazia juu ya nyimbo hizo.

Soma Pia: Rosa Ree, Frida Amani na Chemical Waingia Studio Kutengeza Wimbo wa Pamoja

JIpinde - Ibraah

Chinga amerudi tena kwenye muziki na kibao chake kipya cha ‘Jipinde’ ambacho kimeandaliwa na Bboy Beats. ‘Jipinde’ inamuonesha Ibraah akiwa anamsifia mpenzi wake. Wimbo huu umepata mwitikio mkubwa sana kwa mashabiki kwani ndani ya masaa 15 ilikuwa ishatazamwa mara Milioni moja.

https://www.youtube.com/watch?v=buiRt-we5SI

Songi Songi - Maudi Elka ft Alikiba

Kwa mara nyingine tena bosi wa Kings Music anaonesha utashi wake wa kuimba kwa lugha ya kifaransa kwenye wimbo huu alioshirikishwa na Maudi Elka kutokea Congo. Wimbo huu umepokelewa kwa mikono miwili na wana Afrika Mashariki na kufikia sasa umeshatazamwa mara laki saba thelathini na tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=X1-vDQIrBCU

Zuchu - Yalaaaa

Zuchu anaendelea kuachia burudani maridhawa kwa shabiki zake baada ya kutoa wimbo wake wa ‘Yalaaaa’ uliotayarishwa na Mocco Genius. Zuchu anatumia mdundo uliopambwa na ala za muziki kama madufu na filimbi kupeleka salamu duniani kuwa yeye ametokea visiwani Zanzibar. Kufikia sasa wimbo huu ushatazmawa mara Laki tano arobaini na mbili huko YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=oPSnQ2BhxCI

Naanzaje - Diamond Platnumz

Baada ya kupagawisha mashabiki na ‘Iyo’, Diamond Platnumz anaendelea kujiongezea nafasi kwenye mioyo ya mashabiki kwa kuleta ‘Naanzaje’. Huu ni wimbo ambao umefuata miiko na sheria zote za muziki mzuri. Kwenye wimbo huu Platnumz anaonesha namna ambavyo anampenda na kumthamini mpenzi wake. Kufikia sasa ‘Naanzaje’ ushatazamwa mara laki sita sabini kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=DxQXlXDok34

Happy Birthday - Rayvanny

Rayvanny aliamua kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kuachia wimbo wake unaoitwa ‘Happy Birthday’. Kilichovutia zaidi ni video ya wimbo huu ambayo imehusisha mastaa tofauti tofauti hapa nchini Tanzania kama vile Mbosso, Bahati, Jux, Dulvanny, Paula Kajala na wengineo.

https://www.youtube.com/watch?v=p7U_G7Zt7Ys

Leave your comment