Rosa Ree, Frida Amani na Chemical Waingia Studio Kutengeza Wimbo wa Pamoja

[Picha: Simulizi na Sauti YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Hayawi hayawi sasa yamekua kwani hatimaye rapa kutokea nchini Tanzania Rosa Ree amefanikisha ndoto yake ya kuwakutanisha yeye pamoja na wasanii wa kike wa Hip-hop ambao ni Frida Amani pamoja na Chemical kwenye ngoma moja.

Soma Pia: Zuchu Apigiwa Simu na Rais Samia Akiwa Katikati ya Tamasha lake la Zuchu Homecoming [Video]

Siku chache zilizopita kupitia akaunti yake ya Instagram, Rosa Ree alidokeza kuwa umefika muda muafaka kwa wasanii hao watatu kufanya ngoma ya pamoja na alidokeza kuwa ngoma hiyo ya pamoja inategemewa kuwa kali sana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram sehemu ya Insta story, Rosa Ree alichapisha video zikiwaonesha rappers hao wote watatu wakiwa studio wanaandaa ngoma hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa muziki nchini Tanzania.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na harakati za makusudi za kuwaunganisha wasanii hawa kwenye ngoma moja na bila shaka huu ni ushindi mkubwa kwenye tasnia ya muziki wa Hiphop nchini Tanzania.

Soma Pia; Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Happy Birthday’ [Video]

Kitu cha muhimu cha kukumbuka ni kuwa Rosa Ree yupo mbioni kuachia albamu yake kama ambavyo alitangaza siku chache zilizopita, na ngoma hiyo inatarajiwa kuwepo kwenye albamu hiyo.

Kulingana na Rosa Ree, albamu hio imehusisha wasanii kutokea Kenya, Uganda na Tanzania.

Iwapo Rosa Ree atatoa albamu hio jinsi alivyotangaza hapo awali,  ataweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike wa Hip-hop nchini Tanzania kuwa na albamu.

Leave your comment