Ngoma ya Harmonize ya 'Fall In Love' Yachezwa BET

[Picha: NME]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki kutokea Tanzania Harmonize amedhihirisha kuwa muziki wake umefikia kiwango cha kimatiafa baada ya ngoma yake kuchezwa kwenye kituo cha runinga cha BET.

Ngoma hiyo ambayo imepewa jina la 'Fall In Love' ni mojawapo ya nyimbo zilizoko kwenye albamu ya Harmonize ya Afro East.

Wimbo huo ulichezwa kupitia kipindi cha Afro Soul ambacho kinaangazia miziki za kiafrika.

Soma Pia: Nyimbo Tano Zinazotamba YouTube Tanzania wiki hii

Wimbo wa Harmonize kutambulishwa na kituo cha runinga cha BET ambacho ni cha kimataifa kuna maana kubwa kwa Harmonize kama msanii. Hii pia ni dhihirisho kuwa muziki wa kiafrika umefikia kiwango cha kimataifa na hata kusikizwa na mashabiki walioko bara nyingine.

Tukio hili linatokea siku chache tu baada ya Harmonize kuanzisha ziara yake ya kimuziki Marekani.

Harmonize kupitia ziara hiyo anatarajiwa kutumbuiza mashabiki wake katika mikoa mbali mbali ya Marekani. Harmonize aliambatana na Ibraah ambaye ni msanii aliyesainiwa katika lebo yake ya Konde Music Worldwide.

Soma pia: Killy Aachia "Ni Wewe" Akimshirikisha Harmonize

Ibraah ambaye ni mmoja wa wasanii wanaokuwa kwa kasi mno kutokea lebo hiyo, atakuwa anatumbuiza katika nchi ya kigeni kwa mara ya kwanza. Ziara ya Harmonize kule ulaya inatarajiwa kudumu kwa muda wa miezi miwili.

Aidha, Harmonize pia anatarajiwa kujihusisha na masuala mengine ya kimuziki akiwa Marekani.

Kwa upande mwingine, msanii Diamond Platnmuz ambaye ni bosi wa zamani wa Harmonize pia anatarajiwa kuanzisha ziara yake marekani hivi karibuni. Diamond kwa sasa anashughulikia albamu yake ambayo imesubiriwa kwa hamu sana na mashabiki.

Leave your comment