Killy Aachia "Ni Wewe" Akimshirikisha Harmonize

[Picha: Killy Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Killy kutokea anayefanya vizuri nchini Tanzania ameachia bidhaa mpya sokoni inayokwenda kwa jina la "Ni wewe" akiwa amemshirikisha "Teacher" kutokea Konde Gang Harmonize.

 Killy alidokeza juu ya ujio wa wimbo huu siku chache zilizopita kupitia akaunti yake ya Instagram na siku ya leo ameweza kutimiza ahadi kwa mashabiki zake. "Ni wewe" ni wimbo wa mapenzi na Killy anakiri mapenzi aliyonayo kwa mpenzi na anaonesha ni kwa namna gani anamjali na kumthamini mpenzi na kama unatafuta wimbo ambao utaweka tabasamu usoni kwa mpenzi wako bila shaka Killy ameweza kazi hii kwa ufasaha sana.

Rayvanny Kutangaza Msanii wa Kwanza Kutoka Lebo Yake ya Next Level Music

Killy anafungua kwenye aya ya kwanza ya wimbo huu kwa kuimba "Nabisi nimezaliwa nije nikupende jangwani pakavu kumeota mtende wa ubani wa ubavu sema wapi twende, jua mapenzi ni siri toka enzi zile za mababu" Harmonize anatawala anasikika kwenye aya pili ya wimbo huu akisindikizwa na beat zuri kutoka kwa Hunter ambaye ndiye producer wa wimbo huu.

Kando na wimbo huu Hunter amehusika kutayarisha nyimbo mbalimbali za Konde Gang kama "Jeshi" ya Harmonize pamoja na "Ikune" ya DJ Seven akimshirikisha ndege mnana kutokea Mdee Music Mimi Mars. Huu ni wimbo wa tatu kutoka kwa Killy tangu ajiunge na lebo ya Konde Gang baada ya kuachia Roho mwezi Juni pamoja na "Mwisho" ya mwezi Julai.

https://www.youtube.com/watch?v=ixzllSyWSdU

Leave your comment