Rayvanny Kutangaza Msanii wa Kwanza Kutoka Lebo Yake ya Next Level Music

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Next Level Music Rayvanny hatimaye ametangaza kuwa atamtambulisha msanii wa kwanza aliyesainiwa katika lebo yake muda wowote kuanzia sasa.

Rayvanny hata hivyo hakufichua tarehe kamili ambayo atamtambulisha msanii huyo ambaye amesubiriwa kwa hamu sana.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny na Harmonize Waongoza Wanamuziki wa Bongo Waliotazamwa Zaidi YouTube Mwezi Agosti

Tangazo hilo linatokea wakati ambapo Rayvanny kwa siku za hivi karibuni amekuwa akikumbana na swali la yeye kuchelewesha kumtoa msanii wake wa kwanza.

Licha ya Rayvanny kuzindua lebo yake ya Next Level Music, bado hajamtambulisha msanii yeyote aliyemsaini. Rayvanny hata hivyo mara kwa mara amejitetea kwa kusema kuwa anafanya kazi kwa kufuata utaratibu wake na usimamizi wa lebo hiyo.

Alisisitiza kuwa hataki kumtoa msanii kwa kukurupuka au kwa sababu ya shinikizo zilizoko mtandaoni. Alieleza kuwa anataka kumtoa msanii ambaye ataweza kujinufaisha kimuziki na pia kuweza kusaidia familia yake.

Soma Pia: Rayvanny Adai Alikiba ni Fundi Bora wa Muziki Kuliko Harmonize

Aliongeza kuwa hataki kuwatoa wasanii ili aonekane ako na vijana wengi. Rayvanny hata hivyo alikwisha wahakikishia mashabiki wake kuwa mikakati yote katika Next Level Music tayari ishakamilika na kilichosalia ni kumtambulisha msanii wake wa kwanza.

Licha ya kuwa Rayvanny ameanzisha lebo yake, yeye bado ni mwanachama wa WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz. Bado haijafahamika iwapo WCB itanufaika kimapato kutoka kwa Next Level Music.

Kwa sasa, macho yote yako kwake Rayvanny huku mashabiki wakisubiri kuona msanii atakayetambulishwa.

Leave your comment