Diamond, Rayvanny na Harmonize Waongoza Wanamuziki wa Bongo Waliotazamwa Zaidi YouTube Mwezi Agosti
1 September 2021
[Picha: Ghafla]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mwezi Agosti umeisha na hatimaye tumeingia Septemba na kwenye kiwanda cha muziki, majukwaa mbalimbali kama YouTube huwa na utamaduni wa kufunga mahesabu kuhusu msanii gani amefanya vizuri ndani ya mwezi husika.
Soma Pia: Zuchu Aeleza Mbona Diamond Hakuhudhuria Tamasha la Zuchu Homecoming
Kulingana na taarifa za YouTube, wafuatao ni wasanii watano ambao wamepata watazamaji wengi sana YouTube kwa mwezi Agosti.
Diamond Platnumz
Bosi huyu wa lebo ya WCB anashikilia usukani mwezi huu na ametazamwa mara milioni thelathini na tatu nukta tisa. Ndani ya mwezi huo, Diamond Platnumz aliachia wimbo wa ‘Naanzaje’ ambao kufikia sasa umetazamwa mara milioni mbili nukta moja kwenye mtandao wa YouTube.
Soma Pia: Mbinu Alizotumia Diamond Platnumz Kufikisha Watazamaji Bilioni 1.5 Kwenye YouTube
Rayvanny
Chui kutokea Next Level Music ametazamwa mara milioni ishirini na tatu nukta nne kwenye mtandao wa YouTube, hivyo kushikilia namba mbili. Bila shaka, Rayvanny anastahili kupata idadi hii ya watazamaji kwani ndani ya mwezi Agosti ametoa video ya ‘Sweet’ , ‘Chawa’ na video mbili za nyimbo yake ya ‘Happy Birthday’ ambazo zimefanya vizuri sana
Harmonize
Kwa sasa Tanzania inamfahamu kama ‘Teacher’ na ualimu wake hauishii kwenye Amapiano tu bali hata YouTube. Mwezi Agosti, chaneli ya Harmonize ilitemebelewa mara milioni kumi na sita nukta saba. Ndani ya mwezi Agosti, Harmonize alitoa video ya ‘Mang'dakiwe Remix’ na ilipofika Agosti 30 Konde Boy aliachia video ya ‘Teacher’.
Mbosso
Mbosso Khan anakaa namba nne kwa mwezi Agosti na ametazamwa mara milioni kumi na tano nukta saba. Mbosso alichangamsha Mwezi Agosti baada ya kutoa video mbili ‘Your Love’ na ‘Tulizana’ ndani ya siku moja
Zuchu
Mwanamuziki huyu kutokea WCB ndani ya mwezi Agosti pekee ametazamwa mara miliono kumi na tatu nukta nne. Ndani ya mwezi Agosti Zuchu alitoa wimbo wake wa ‘Yalaaaa’ ambao kufikia sasa audio imefikisha watazamaki takriban laki tano.
Leave your comment