Zuchu Aeleza Mbona Diamond Hakuhudhuria Tamasha la Zuchu Homecoming

[Picha:Top Naija]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki kutokea lebo ya WCB Zuchu ameleza kwanini bosi wake Diamond Platnumz hakuhudhuria tamasha lake la Zuchu Homecoming, iliyofanyika Zanzibar wikendi iliyopita.

Soma Pia: Nyimbo 5 Mpya za Rayvanny, Alikiba, Ibraah, Zuchu na Harmonize Zinazotamba Tanzania Wiki Hii

Katika mahojiano na Wasafi TV, Zuchu alionyesha mazungumzo yake ya kibinafsi na Diamond ili kwajibu mashabiki waliokuwa na viulizo vya mbona Diamond hakujitokeza kumuunga mkono msani wake.

Katika mazungumzo hayo waliofanya kwenye mtandao wa WhatsApp, Diamond alieleza kuwa hakutaka kuenda kwa tamasha la Zuchu Homecoming kwa sababu hakutaka kuiba nyota ya Zuchu. Alisema kuwa kama yeye angeenda na kutumbuiza, basi yeye ndiye angekuwa gumzo na si Zuchu.

Soma Pia: Zuchu Adhibitisha Uwepo wa Kolabo Nyingine Baina Yake na Rayvanny

Diamond aliendeleza maelezo yake kwa kusema kuwa aliwaambia wasanii wengine wa WCB wakiwemo Lavalava na Mbosso kuenda bila ya kusema ili wampee nafasi Zuchu kuweza kung'aa zaidi kwani lilikuwa tamasha lake kibinafsi kama msanii.

"Doris (meneja wa Zuchu) and the whole team have been calling me back to back, boss please come. I told them leo ni siku yako, unatakiwa ustand out, tukuache ushine. Nikija story zote zinahama, inakuwa si Zuchu tena ni habari ya Diamond. Na unanijua nikija sinanga show ndogo, ila now habari imebaki kuwa ni Zuchu," ujumbe wa Diamond katika mazungumzo yake na Zuchu ulisomeka.

Leave your comment