Nyimbo 5 Mpya za Rayvanny, Alikiba, Ibraah, Zuchu na Harmonize Zinazotamba Tanzania Wiki Hii

[Picha: SoundCity TV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tabasamu linaendelea kutawala kwa wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva kwani wasanii kutokea nchini Tanzania wanaendelea kutoa kazi kali na kati ya hizo kuna nyimbo ambazo zimevuma sana hasa kwemye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Kolabo Tano Kali Zilizohusisha Wasanii wa Tanzania na Kenya

Nakala hii inaangazia nyimbo tano ambazo zinatamba sana kwenye mtandao wa Youtube kwa wiki hii.

Jipinde - Ibraah

Kwa wiki ya pili mfulullizo Ibraah anaendelea kufanya vizuri na ‘Jipinde’ ambayo imeandaliwa na Bboy Beats. Kufikia sasa wimbo huu umetazamwa mara milioni mbili nukta nne kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=buiRt-we5SI

Songi Songi Remix - Maudi Elka ft Alikiba

Sauti nzuri ya Alikiba pamoja na lugha ya kifaransa aliyotumia ndani ya wimbo huu bila shaka ndio vitu vilivyofanya wimbo huu upokelewe kwa mikono miwili na mashabiki. Kufikia sasa wimbo huu ushatazamwa takriban mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=lUllXZIQLzY

Happy Birthday - Rayvanny

Ni jambo jema mno kutakiana kheri katika kumbukizi ya siku zetu za kuzaliwa na katika kulitambua hilo Rayvanny aliachia wimbo wa ‘Happy Birthday’ ili uweze kuburudisha watu pindi wanaposheherekea siku zao za kuzaliwa. Kilichopendezesha zaidi kazi hii ya Rayvanny ni kushirikisha wasanii tofauti tofauti kwenye video ikiwemo Paula Kajala, Whozu, Dulivani, Mbosso, Gigi Money, Young Lunya na wengineo.

https://www.youtube.com/watch?v=jyfS60NKWNI

Mang'dakiwe Remix - DJ Obza, Harmonize & Leon Lee

Kwa sasa tunaweza sema Harmonize ni nembo ya muziki wa Amapiano hapa nchini Tanzania. ‘Mang'dakiwe Remix’ inaendelea kuthibitisha hilo kutokana na kufanya vizuri sana huku video ya wimbo huo ikiwa imepambwa na dansi mujarab kabisa kutoka kwa watu wa Konde Gang. Kufikia sasa wimbo huo umetazamwa mara Milioni tatu nukta nane kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=EK8y4hcrJyA

Yalaaaa - Zuchu

Baada ya kutupumzisha kwenye ‘Nyumba Ndogo’, Zuchu amerudi tena na ngoma yake ya  ‘Yalaaaa’. Kwenye wimbo huu Zuchu, anakiri dhahiri shahiri kuwa penzi limemzidia kiasi cha kuomba msaada kutoka serikalini na ili kuweza kukuza wimbo huu. Zuchu ametoa video ya dansi ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara laki nane kumi na nne kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=oPSnQ2BhxCI

Leave your comment