Kolabo Tano Kali Zilizohusisha Wasanii wa Tanzania na Kenya

[Picha: Kiza Kinene Video]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tanzania na Kenya ni majirani wa muda mrefu sana na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umegonga hodi mpaka kwenye kiwanda cha muziki ambapo wasanii kutoka nchi hizo aghalabu hufanya nyimbo kwa pamoja.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo na Wasanii Diamond, Rayvanny, Zuchu na Ibraah

Makala hii inaangazia nyimbo tano ambazo wasanii kutokea nchini Tanzania na Kenya wamefanya kwa pamoja:

Kiss - Bahati ft Rayvanny

Huu ni wimbo namba mbili kwenye albamu ya ‘Love Like This’ ambayo imeweza kufanya vizuri sana hapa Afrika Mashariki. Bahati anamshirikisha Rayvanny kutokea lebo ya Wasafi na wimbo huu umeandaliwa na mtayarishaji Sav Beats. Ilimlazimu Bahati kuja mpaka Dar Es Salaam nchini Tanzania ili aweze kukamilisha video ya wimbo huu.

https://www.youtube.com/watch?v=RM2GGAtvn9g

Warembo - Lavalava ft Susumila

Kama unataka kusikia sifa za warembo kutokea Tanzania na Kenya basi huu wimbo ni kwa ajili yako. Kwenye wimbo huu, Lavalava na Susumila wanapeana zamu kuzungumzia sifa za warembo waliopo Tanzania na Kenya. Kibao hiki kimetayarishwa na Monsta Madness huku video ikiongozwa na Kevin Bosco kutokea nchini Kenya.

https://www.youtube.com/watch?v=qRixDqzpypo

Hello Baby - Avril ft Ommy Dimpoz

Bila shaka ‘Hello Baby’ ni moja kati ya nyimbo bora za mwaka 2015 kwani mashabiki wa muziki waliupokea wimbo huu kwa ukubwa sana. Kwenye mtandao wa YouTube, wimbo huu umeshatazamwa takriban mara Milioni 2 nukta nne. Video ilifanyika nchini Kenya kwenye eneo zuri la Naivasha huku wimbo ukitayarishwa na Manwater kutoka nchini Tanzania na Ogopa Deejays kutokea Kenya.

https://www.youtube.com/watch?v=EDmKnqpdw1k

Gere - Tanasha Dona ft Diamond Platnumz

Pale wapendanao wawili wanapoamua kushirikiana basi hakuna linaloharibika na hilo lilithibitishwa na Tanasha Donna baada ya kumshirikisha Diamond Platnumz kwenye wimbo huo. Lizer Classic kutokea Wasafi Records ndiye amehusika katika kutengeneza audio ya wimbo huu. Kufikia sasa, wimbo huu umeshatazamwa Milioni 27 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=z9b4_2lBhrE

Kiza Kinene - Nandy ft Navy Kenzo

 Ilipofika mwezi Septemba 2019, Nandy aliweka rekodi mpya kwenye muziki wake baada ya kuachia wimbo wa Kiza Kinene akishirikisha kundi la Sauti Sol kutokea nchini Kenya. Kiza Kinene ni wimbo unaozungumzia wapenzi wawili ambao waliamua kuachana kutokana na maneno ya watu. Bila shaka, Kimambo Beats ambaye ndiye mtayarishaji wa wimbo huu aliweza kutengeneza kibao kikali ambacho kiliwaburudisha vyema wana Afrika Mashariki.

https://www.youtube.com/watch?v=FcAjVCy-m7s

Leave your comment