Nyimbo Tano Zinazotamba YouTube Tanzania wiki hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kama wewe ni shabiki wa na unataka kujua ni nyimbo gani zinasikilizwa sana nchini Tanzania kwa wiki hii basi umefika sehemu sahihi kwani makala hii inalenga kukupitisha mwenye nyimbo tano zinazofanya vizuri Tanzania kwenye mtandao wa Youtube wiki hii.

Rais wa Kitaa - Nay Wa Mitego.

Nay Wa Mitego anaendelea kudhihirisha kuwa yeye ni kipaza sauti cha watanzania kupitia wimbo wake mpya ambao umezua gumzo nchini Tanzania kwani ameongelea vitu vinavyogusa maisha halisi ya watu kama tozo za simu, mfumuko wa bei na hali ya kisiasa ilivyo nchini Tanzania. Kufikia sasa wimbo huu umetazamwa mara laki nane ishirini na nne elfu kwenye mtandao wa Youtube. 

https://www.youtube.com/watch?v=0AEyaLhZR8E

Teacher - Harmonize

Mwalimu mkuu kutokea shule ya muziki ya Konde Gang ameendelea kufanya vizuri na wimbo wake wa "Teacher" ambao ndani yake Tembo ameelezea namna ambavyo anachanua kwenye soko la muziki nchini Tanzania kiasi cha washindani kuanza "Kumgeza" Video ya kimataifa ya wimbo huu ambayo imepambwa na miondoko matata ya dansi imeongozwa na Director Ivan kutokea Tanzania na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 2 nukta nane kwenye mtandao wa Youtube. 

https://www.youtube.com/watch?v=mPVoKSc6LJo

Jipinde - Ibraah

Mwana wa mfalme kutokea himaya ya Konde Gang Ibraah anaendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya "Jipinde" ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 2.7 kwenye mtandao wa Youtube. Mashabiki wameonekana kuikubali vilivyo ngoma hii kwani iliweka rekodi mpya kwenye muziki wa Ibraah kwa kutazamwa mara Milioni 1 ndani ya saa 15 tu kwenye mtandao wa Youtube. 

https://www.youtube.com/watch?v=buiRt-we5SI

Happy Birthday - Rayvanny.

Ili kuweza kuadhimisha kumbukizi ya siku ya siku yake ya kuzaliwa, Rayvanny alichomoa wimbo wa "Birthday" kutoka kwenye maktaba yake ya muziki na kuwapa shabiki zake kama zawadi. Mdundo wa kuchangamka ulioandaliwa na Trone umefanya ngoma hii kuwa bora sana huku video ya wimbo ikiwa imehusisha mastaa kadhaa kutokea Tanzania na kufikia imeshatazamwa mara Milioni 1 nukta mbili. 

https://www.youtube.com/watch?v=jyfS60NKWNI

Naanzaje - Diamond Platnumz

Ilipofika Agosti 22 Diamond Platnumz aliachia wimbo wake wa tatu kwa mwaka huu unaoitwa "Naanzaje". Wimbo huo umepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa muziki kutokea nchini Tanzania ambao kwa muda mrefu walikuwa wana hamu ya kusikia ladha ya Bongo Fleva kutoka kwa Diamond Platnumz na kufikia sasa video hio imeshatazamwa takriban mara Milioni 1 nukta mbili kwenye mtandao wa Youtube .

https://www.youtube.com/watch?v=iKbW2EDs_mE

Leave your comment