Nyimbo Tano Kali Kutoka Kwa Rapa Dogo Janja

7

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Jina lake halisi ni Abdul Aziz Chande na alizaliwa Septemba 15 mwaka 1994 huko jijini Arusha eneo la Ngarenaro na ulipofika mwaka 2009, ndipo Dogo Janja akiwa na umri wa miaka 15 tu aliingia rasmi kwenye tasnia ya muziki baada ya kukutana na Madee kutokea Tiptop Connection.

Soma Pia: Dogo Janja Aeleza Sababu ya Kuwashirikisha Wasanii wa Kike Pekee Kwenye Albamu Mpya ‘Asante Mama’

Tangu mwaka 2009 mpaka sasa, Dogo Janja amejitengenezea jina na wasifu mkubwa kwenye muziki wa Hip-hop. Kwa sasa, ukitaja orodha ya marapa wakali kutokea Tanzania kisha ukaruka jina la Dogo Janja bila shaka watu wa Ngarenaro mji ambao anatokea staa huyu hawatakuelewa hata kidogo.

Siku ya leo Septemba 15 akiwa anatimiza miaka 27, ili kuadhimisha kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa zifuatazo ni nyimbo tano kali kutoka kwa rapa huyo.

Ngarenaro

Kuna muda unapata mpenzi ambaye ukikaa ukifikiria unaona ni kama umeokota dodo chini ya mwembe. Ngoma ya ‘Ngarenaro’ ya Dogo Janja imeelezea kwa undani dhana hiyo. Kwenye wimbo huu Dogo Janja anaelezea kinaga ubaga namna ambavyo anamzimikia mpenzi wake kiasi cha kutokuamini kuwa ni wa kwake.

https://www.youtube.com/watch?v=YlqpDGO1TUQ

Kidebe

Huu ni wimbo wa kusherehekea mapenzi ya watu wawili ambao wamedumu kwa muda mrefu kwenye mahusiano. Kipindi ngoma hii inatoka kila sehemu kuanzia kwenye runinga, redio pamoja klabu ngoma hii ilikuwa inasikika.

https://www.youtube.com/watch?v=62EjMufcvHM

Ukivaaje Unapendeza?

Kama unapenda mitindo mipya ya fasheni na umaridadi kwenye kuvaa Dogo Janja ilipofika Mei mwaka 2017 alitoa ngoma yake ya "Ukivaaje Unapendeza". Ngoma hii imegusia zaidi kuhusu mavazi na humu ndani Dogo Janja anajisifia namna ambavyo yeye ni bingwa kwenye suala zima la kuvaa na kupendeza kuliko msanii yeyote yule.

https://www.youtube.com/watch?v=XjiiZBeXHiU

My Life

Kwenye ‘My Life’ Dogo Janja anazungumzia mambo ya ‘kiutu uzima sana’ kwani anatoa mafundisho kama matumizi mazuri ya pesa, uaminifu na kujipenda mwenyewe. Kama utamaduni wa Hip-hop ulivyo, Dogo Janja hasahau kujisifia mwenyewe.

https://www.youtube.com/watch?v=PGxLp4v1aYE

Banana

Kama unatafuta wimbo ambao utacheza bila kutumia nguvu nyingi basi ngoma ya ‘Banana’ itakufaa sana. Kazi nzuri ya mtayarishaji wa muziki Kimambo Beats imefanya wimbo huu ulioingia sokoni mwaka 2018 kuwa na hadhi ya kimataifa. Kufikia sasa video ya wimbo huu imeshatazamwa mara Milioni 2.6 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=hnSS7vkcka8

Leave your comment