Dogo Janja Aeleza Sababu ya Kuwashirikisha Wasanii wa Kike Pekee Kwenye Albamu Mpya ‘Asante Mama’
5 July 2021
[Picha: Dogo Janja Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Msanii kutokea nchini Tanzania Dogo Janja ameeleza kwa undani kwanini albamu yake ya ‘Asante Mama’ alioitoa hivi karibuni ameshirikisha wasanii wa kike pekee. Dogo Janja alifunguka hivi karibuni na kusema "Kitu cha kwanza ni kuleta utofauti katika albam kwa sababu sidhani kama duniani imewahi kufanyika na hata kama imefanyika basi itakuwa ni mbali sana".
Soma Pia: Rayvanny, Guchi Waanza Harakati za Kuachia Video ya ‘Jenniffer Remix’
Dogo janja ambaye alianza harakati zake za muziki tangu akiwa mdogo, Juni 4 mwaka huu alitoa albamu iitwayo ‘Asante Mama’ akiwashirikisha wasanii kama Lulu Diva, Patricia Hillary, Linah Sanga, Rosa Ree, Nandy, Khadija Kopa, Mimi mars, Maua sama na Lady Jaydee.
Dogo Janja aliongeza kwa kusema pia albamu yake imepata mapokezi mazuri kutoka kwa wapenzi wa muziki wake na ni suala la muda tu yeye kuanza kuachia video za nyimbo zote zilizopo kwenye albamu yake.
Soma Pia: Rayvanny Kumtambulisha Msanii wake wa Kwanza Hivi Karibuni
"Mapokezi yamekuwa mazuri, ilianza kwenye platform moja lakini sasa inapatikana kwenye platform zote so sa hii tunaenda kupush ikifika malengo tuliokuwa tunataka nadhani tutaanza video, tutaanza kurelease video za kwenye albam" alisema msanii huyo.
Sambamba na hilo, Dogo Janja aliweka wazi kuwa hayuko tayari kubadilisha jina lake hata kama umri wake ni mkubwa kwani kufanya hivyo kutaharibu biashara ya muziki wake huku akimtolea mfano msanii Aslay ambaye hakuangaika kubadilisha jina ila watu walizoea tu wenyewe.
"Mimi ni forever Young. Dogo Janja tayari imekuwa ni brand, ni biashara ambayo iko sokoni. Watu watazoea wenyewe kama Aslay hajaangaika kutumia nguvu imekuja tu automatically," alisema Dogo Janja.
Leave your comment