Rayvanny, Guchi Waanza Harakati za Kuachia Video ya ‘Jenniffer Remix’
2 July 2021
[Picha: Rayvanny Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mkurugenzi mkuu wa Next Level Music Rayvanny amemsifu msanii Guchi kutoka Nigeria, na kumtaja kama msanii mwenye talanta na kazi za kupendeza.
Rayvanny na Guchi hivi majuzi waliachia wimbo mpya kwa jina ‘Jennifer Remix’. Toleo asili la wimbo wa ‘Jeniffer’ lilitayarishwa na Guchi na lilipokelewa vyema na mashabiki. Ushirikiano kati ya Guchi na Rayvanny kwenye remix ya wimbo pia umepokelewa na mashabiki wao.
Soma Pia: Rayvanny Kumtambulisha Msanii wake wa Kwanza Hivi Karibuni
Katika harakati za kuandaa video, Guchi alitua Tanzania Alhamisi, tarehe mosi, mwezi wa Julai na akapokelewa na Rayvvanny.
Rayvanny akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege alipomkaribisha Guchi, alifichua kuwa msanii huyo yuko nchini ili waandae video ya remix hio.
Rayvanny pia aliweka wazi kuwa atamshirikisha Guchi katika miradi mingine, na kuongeza kwamba aliamua kufanya kazi na Guchi kwa sababu yeye ni mwanamuziki anayejituma na hutoa muziki mzuri.
Soma Pia: Rayvanny Amtetea Diamond Platnumz Baada ya Kukosa Tuzo la BET
Kulingana na Rayvanny, mashabiki wanapaswa kutarajia nyimbo kadhaa kutoka kwake na Guchi.
"Mimi najua muziki mzuri na kila mtu anajua mziki mzuri. Wimbo huo nilikua naupenda sana lakini yeye mwenyewe pia baada ya kuongea naye akasema yes kwa sababu tunataka kufanya kazi nyingine akasema no, tuanze na remix ya Jeniffer kwanza," Rayvanny alisema.
Kwa upande wake, Guchi alisema kuwa anapenda midundo za nyimbo za kibongo na amekuwa na ndoto ya kufanya kazi na wanamuziki wa Kitanzania. Pia alisema kuwa mtindo wake wa muziki karibu unafanana na ule wa bongo.
Leave your comment