Alikiba Afichua Sababu Kuu Iliyochelewesha Albamu Yake

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutokea Tanzania Alikiba hatimaye amefunguka kuhusu kuchelewa kwa albamu yake ambayo imesubiriwa kwa hamu sana na mashabiki.

Soma Pia: Alikiba Afunguka Jinsi Alivyoguswa na Shabiki Aliyempa Zawadi ya Mchoro ya Babake

Hapo awali Alikiba alitangaza kuwa ataachia albamu yake mwaka huu kabla ya mwezi wa Julai. Licha ya kuweka wazi tangazo hilo, albamu hiyo haikutoka na hivyo basi kuibua maswali miongoni mwa wafuasi wake.

Alikiba kupitia video aliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram, alieleza kuwa albamu hiyo imechelewa kwa sababu ya kolabo ambazo amezifanya humo ndani.

Soma Pia: Zuchu Atangaza Ujio wa Simulizi ya Safari Yake ya Muziki

Alisema kwa sasa yeye pamoja na timu yake wanashughulikia kumalizia kolabo hizo kabla albamu hiyo haijatoka. Msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Kings Music hata hivyo hakufichua habari kuhusiana na wasanii ambao ameshirikiana nao kwenye albamu hiyo.

 

Aidha, Alikiba aliongeza kuwa albamu hiyo itatoka baada ya mwezi mmoja.

 

"Album inatoka in 30 days. Kuna collaborations ambazo tulizofanya zimedelay kumalizika. Nami mtangazaji wenu kutoka official Alikiba," Alikiba alisema wakati akiwaburudisha mashabiki wake mtandaoni.

Albamu yake Alikiba imesubiriwa sana na imeibua hisia tofauti katika tasnia ya muziki ya Tanzania. Hii ni kutokana na kuwa mpinzani wake mkuu Diamond Platnumz pia anatarajiwa kuachia albamu pia.

 

Diamond aliwahi safiri kuelekea marekani katika shughuli za kutayarisha albamu yake. Albamu hizi mbili zinatarajiwa kuzua kivumbi bongo kwani mabingwa hao wawili ambao pia ni wahasimu wa jadi watakua uwanjani kubaini nani fundi wa muziki kumshinda mwengine.

Leave your comment