Alikiba Afunguka Jinsi Alivyoguswa na Shabiki Aliyempa Zawadi ya Mchoro ya Babake

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Safari ya msanii katika muziki hung'aa zaidi kutokana na upendo wa mashabiki wao. Mara kwa mara, mashabiki hutumia mbinu tofauti kuonyesha upendo wao kwa wasanii. Kuna wale ambao huhudhuria tamasha zilizoandaliwa na wasanii kama njia ya kuwaonyesha upendo, na vilevile kuna wale ambao huchukua hatua zaidi na kuwapa zawadi kibinafsi.

Soma Pia: Zuchu Afichua Siri Iliyofanikisha Tamasha lake la Zuchu Homecoming

Mwanamuziki tajika kutoka Tanzania Alikiba hivi maajuzi alikuwa mwingi wa hisia na hata kutokwa na machozi alipopewa zawadi na shabiki wake. Zawadi hiyo ilikuwa picha ya babake mzazi iliyochorwa kwa mkono.

Video iliyoonyesha Alikiba akilia baada ya kuona mchoro huo ilisambaa mtandao na kuibua hisia miongoni mwa mashabiki wake huku wengi wakimtuliza. Aidha, Alikiba hatimaye amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram na kutoa maelezo ya zawadi hiyo. Alikiba alikiri kuwa kamwe hakutegemea zawadi ya mchoro wa babake marehemu, huku akiongezea kuwa mara mingi yeye hupata zawadi ya michoro yake.

Soma Pia: Kolabo Tano Kali Zilizohusisha Wasanii wa Tanzania na Kenya

Alisema kuwa ataithamini kazi ya wasanii wanaochukua muda wao kusudi kumuonyesha upendo.

"Nimekutana na mashabiki wengi wanaopenda muziki wangu mimi huwaita #Alikibloodfans, wao hunipa zawadi mbalimbali na moja ya zawadi kubwa nayopewa na wengi wao ni picha za kuchora kwa mkono nyingi zikiwa zangu, Nilipata zawadi hii kutoka kwa @ymakenya, alimchora Baba yangu mzazi ambaye hatuko nae tena duniani, ni kitu ambacho sikutegema wala kufikiria kabisaa!

"Nashukuru sana kwa zawadi hii ambayo kwangu ni ya kipekee sana. Siku zote nitathamini na kushukuru kila mtu anaechukua muda wake kufanya kazi hii ya sanaa na kuonesha upendo kwangu !! Mwenyezi Mungu awazidishie baraka zake katika kazi zenu," chapisho la Alikiba mtandaoni lilisomeka.

Leave your comment