Zuchu Afichua Siri Iliyofanikisha Tamasha lake la Zuchu Homecoming

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tamasha la Zuchu Homecoming lililofanyika mnamo tarehe 21 mwezi Agosti lilikuwa mojawapo ya matamasha makubwa sana kuwahi kufanyika mkoani Zanzibar.

Tamasha hilo lilivutia watu wengi kwa kiasi ya kuijaza uwanja wa Imani. Kikubwa zaidi ni kuwa tamasha hilo lililoandiliwa na msanii tajika kutoka WCB Zuchu, lilivutia hadi rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Soma Pia: Zuchu Adhibitisha Uwepo wa Kolabo Nyingine Baina Yake na Rayvanny

Lakini Je, ni nini haswaa iliyofanikisha tamasha hiyo ikizingatiwa lilikuwa tamasha la kwanza kuandaliwa na Zuchu kama mwanamuziki?

Zuchu katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni alifichua siri iliyompa mafanikio hayo. Akizungumza na Simulizi na Sauti, Zuchu alisema kuwa kikubwa kilichomfanya kujaza uwanja wa Imani ni kuwa wazanzibari wanampenda kwa sababu yeye alizaliwa na kulelewa Zanzibar.

Kulingana na mwanahabari aliyekuwa akimhoji Zuchu, mara mingi huwa ngumu sana wasanii haswaa wale kutoka bara kuweza kuvutia wazanzibari katika tamasha zao. Aidha, Zuchu aliongeza kuwa kulingana na takwimu zilizotokana na utafiti wao, anashabikiwa sana Zanzibar ikilinganishwa na sehemu zingine za Tanzania.

Soma Pia: Ujumbe wa Zuchu Kwa Mashabiki Baada ya Tamasha Lake Kupata Mafanikio

"Ofisini kuna statistics za kila msanii anavyofanya. Mimi nasapotiwa sana obviously Tanzania, inafuata Kenya, zinafuata nchi kama Maskati sijui nini. Yaani pale tunaona statistics. Kwa ile Tanzania tukiangalia almost Zanzibar nzima inanisapoti," Zuchu alisema.

Zuchu kwa sasa ni mmoja wa wasanii wa kike wanaotamba katika tasnia ya muziki ya Tanzania.

Zuchu amesifiwa sana kutokana na mafanikio yake makubwa ndani ya muda mfupi kwenye muziki.

Ngoma aliyoachia hivi maajuzi kwa jina la 'Yalaaaa' ndio ingali inampeperusha katika anga za burudani.

Leave your comment