Zuchu Atangaza Ujio wa Simulizi ya Safari Yake ya Muziki

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutokea lebo ya WCB Zuchu ametangaza kuwa hivi karibuni ataachia simulizi ya safari yake ya muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu alisema kuwa tayari amekamilisha asilimia sabini ya simulizi hiyo. Aliongeza kuwa amekua akijihusisha pakubwa katika kufanikisha simulizi hiyo kwa siku za hivi karibuni.

Soma Pia: Zuchu Achochewa Kuongeza Bidii Baada Ya Tems Kushirikishwa Kwenye Albamu Ya Drake

Kikubwa kilichosalia ili simulizi hiyo ikamilike ni uwepo wa wasimamizi wake. Katika simulizi hiyo, Zuchu atawahadithia mashabiki wake kuhusu maisha yake kabla hata hajaingia kwenye tasnia ya muziki hadi alipo sasa.

Zuchu hata hivyo aliomba kuwashirikisha mashabiki wake katika kuipa simulizi hiyo jina huku akiahidi kuwa yeyote atakeyotoa jina la kuridhisha atahusishwa kwenye simulizi hiyo.

Soma Pia: Zuchu Ajivunia Kutokana na Mafanikio Yake Makubwa Kimuziki

"My documentary is 70% ready Niko busy kumalizia documentary yangu kwa muda sasa .Na niseme tu Nasubiria uwepo wa maboss zangu umalizike watoe ushuhuda wao then itakua tayari kwa asilimia 100%," Zuchu aliandika mtandaoni.

"Humu Kuna maisha yangu ya kabla na baada nimeweka safari yangu nzima Mpaka hapa nilipo sasa .Kwenye documentary hii Naomba nishirikiane nanyi kwenye upande wa Jina .Nyinyi mashabiki zangu mko nami tangu natoka hivyo basi nadhani kwa kufatilia safari yangu Mnaweza kunipa Jina Sahihi la hii documentary.Ataetoa Jina ni lazima Atalipwa na kutambulika kama mmoja wa washiriki kwenye Documentary hii," aliongezea.

Zuchu kwa sasa ni miongoni mwa wasanii wakubwa wanaopeperusha bendera ya Tanzania kimuziki. Licha ya kuwa kwenye tasnia hii kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitano, tayari Zuchu amepanda ngazi na kuwa msanii anayeheshimika sio Afrika Mashariki tu bali Afrika nzima.

Leave your comment