Zuchu Ajivunia Kutokana na Mafanikio Yake Makubwa Kimuziki

[Picha: Nairobi News]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki kutokea lebo ya WCB Zuchu amejitokeza na kujivunia maendeleo yake ya muziki haswaa baada ya tamasha lake la Zuchu Homecoming kupata mapokezi mazuri.

Zuchu katika taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagam aliashiria kuwa moja wapo ya siri ya mafanikio yake kama mwanamuziki ni kutokata tamaa katika kufuata ndoto yake.

Soma Pia: Nyimbo Tano Zinazotamba YouTube Tanzania wiki hii

Alijivunia kuwa licha ya kuwa kwenye tasnia ya muziki kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitano tayari ameweza kufanikisha tamasha kubwa liliohudhuriwa na watu wengi sana.

Tamasha la Zuchu Homecoming lililofanyika mkoani Zanzibar mwezi wa nane mwaka huu ndilo lilikuwa tamasha la Zuchu la kwanza kuliandaa kama mwanamuziki.

Zuchu pia alidokeza kuwa kuna uwezekano akaanda tamasha katika mkoa mwingine. Aliwauliza mashabiki wake wampe maoni ya mkoa mwingine ambao angeenda.

"My homecoming show. Draco said bet on yourself and see how much you grow. Looking back to when I was planning this the challenges were all worth it I learned a lot. Kwako wewe unaesoma hii usikate tamaa inawezakana jiamini wewe kwanza usipojiamini wewe unawapa watu wakati mgumu kukuamini," Zuchu alisema katika chapisho lake.

Soma Pia: Zuchu Achochewa Kuongeza Bidii Baada Ya Tems Kushirikishwa Kwenye Albamu Ya Drake

“1 year and 5 Months in the game and Am already Doing stadiums A show that i Myself arranged Wow," aliongezea.

Zuchu ni mmoja wa wasanii wa kike ambao wanoangoza katika tasnia ya burudani ya Afrika Mashariki. Ameweza kushinda tuzo mbali mbali mojawapo ikiwa tuzo ya AFRIMMA katika kitengo cha Best New Comer Award mwaka wa 2020.

Leave your comment