Zuchu Achochewa Kuongeza Bidii Baada Ya Tems Kushirikishwa Kwenye Albamu Ya Drake

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Tems kutokea Nigeria kwa sasa ni gumzo kubwa sana mitandaoni baada ya habari kuchipuka kuwa atakuwepo kwenye albamu ya rapa wa kimataifa Drake. Habari hizo zimemfikia nyota wa muziki wa bongo Zuchu, ambaye amechochewa kuongeza bidii katika muziki wake ili pia afikie kiwango cha Tems.

Killy Aachia "Ni Wewe" Akimshirikisha Harmonize

Katika taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Zuchu alidai kuwa muziki wa kiafrika unakua na yeye angependa sana kuhusika katika kuendeleza tasnia ya muziki ya Afrika.

 Zuchu hata hivyo alitupia dongo mashindano baina ya wasanii ambayo alisema kuwa ni ya ujinga. Msanii huyo ambaye amesainiwa katika lebo ya WCB, aliendelea kwa kumpongeza Tems kwa mafanikio yake.

 "All these stupid compititions, this got me motivated. African music is growing and am sure am gonna be part of this growth believe it or not, my studio sessions bout to be. Am going in once again congratulations to Tems," chapisho la Zuchu lilisomeka mtandaoni.

Ikumbukwe kuwa Zuchu ni mmoja wa wasanii wa kike wa bongo ambao wanafanya vizuri sana. Amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa takriban mwaka mmoja na miezi kadhaa, ila mafanikio yake yamezidi muda huo. Amesifiwa na wengi sana kwa jinsi alivyopanda ngazi katika tasnia ya muziki ya Tanzania hadi alipo leo. Kwa sasa Zuchu anatamba hewani na ngoma yake mpya ya 'Yalaaa' ambayo unaweza ukaipata katika tovuti ya Mdundo.com bila malipo.

Leave your comment