Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia ‘Jah Jah’ Akimshirikisha Alikiba

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Tommy Flavour kwa ushirikiano na mwanamuziki nyota Alikiba ameachia wimbo mpya kwa jina 'Jah Jah'.

Katika ngoma hiyo, wasanii hao wanamtukuza na kumsifu Mungu. Tommy Flavour ndiye anachukua mistari ya kwanza ambako anamshukuru Mungu kwa mengi mema aliyotenda maishani mwake.

Soma Pia: Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy Alikiba, Darassa, Harmonize na Rayvanny Watajwa Kuwania Tuzo Za AFRIMA 2021

Alikiba anafuatia katika sehemu ya pili ya wimbo huo na anazungumzia ukuu na mapenzi ya Mungu. Msanii huyo katika upande wake anazungumzia kwa kiasi jinsi Mungu alimwezesha na kumpandisha maishani.

"Oh Baba, Oh Baba. Naomba niongoze. Oh Jah Jah, Oh Jah Jah. Nitakufata nisipotee. Kwenye mabalaa umenipitisha. Kwenye shida na njaa, umenilisha. Wakitaka niende chini wanipandisha. Mapenzi yako siwezi kufananisha," Tommy Flavour anaimba katika utangulizi wa ngoma hiyo.

Soma Pia: Alikiba Apokea Tuzo Mbili Kutoka YouTube

"Oluwa Oh Jah Jah. Wanijua kiundani. Ukinilinda maishani yeah. Sikulipi chochote. Sifuati yako yote. Ila bado ujaniacha, uko na mimi," Alikiba anaimba.

Midundo ya ngoma hiyo imetayarishwa na producer maarufu kutoka Tanzania Yogo Beats. Video kwa upande mwingine imeandaliwa na mwelekezi wa video kutoka nchini Kenya Enos Olik.

Kwenye video hiyo, Alikiba na Tommy Flavour wanaonekana wakiwa pamoja na wenzao wengine waliovalia nguo nyeupe toka mwanzo hadi mwisho. Rangi ya mavazi hayo huenda imetokana na ujumbe uliomo kwenye wimbo huo.

Ngoma hii imepokelewa vyema na imepata maelfu ya watazamaji ndani ya muda mfupi. Wakati wa uchapisho wa nakala hii, ngoma hiyo ilikuwa imetazamwa takriban mara elfu tano.

https://www.youtube.com/watch?v=IM0Rs05yiSw

Leave your comment